1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mizozo yachangia ongezeko la njaa

Oumilkheir Hamidou
15 Oktoba 2019

Faharasa ya shirika la Ujerumani linalopigana dhidi ya njaa-Welthungerhilfe, inasema "hakuna anaebidi kuishi na njaa". Inaaonya mizozo ya mtutu wa bunduki na mabadiliko ya tabianchi inachangia kuzidisha balaa la njaa.

Entwicklungszusammenarbeit | Deutschland | Welthungerhilfe | Demokratische Republik Kongo
Picha: imago images/blickwinkel

 

Shirika la Welthungehilfe linaonya dhidi ya hatari za aina mpya zinazoukabili usalama wa lishe bora kufuatia mabadiliko ya tabianchi katika mataifa ambayo tokea hapo yako hatarini."Juhudi za kupambana na njaa na utapiamlo katika wakati huu wa mabadiliko ya tabianchi zinahitaji kuchukuliwa hatua kali ili kupambana na maafa yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi na wakati huo huo kupunguza madhara yanayotokana na uchafuzi wa mazingira" imetajwa katika faharasa ya mwaka 2019 ya shirika hilo, iliyochapishwa mjini Berlin.

Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita idadi ya watu wanaosumbuliwa na njaa imeanza upya kuongezeka na kufikia watu milioni 882.

Fraser Patterson muasisi wa faharasa hiyo anatoa sababu ya hali hiyo na kusema:"Mambo mawili yamechangia kuongezeka idadi ya watu wanaosumbuliwa na njaa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Kwanza mabadiliko ya tabianchi na pili kuongezeka mizozo ya mtutu wa bunduki."

Katika ripoti yao ya mwaka shirika hilo lisilomilikiwa na serikali linatathmini hali namna ilivyo kuambatana na mambo manne; idadi ya wanaotapiamlo sawa na kuangamia viumbeanuai, kuzorota ukuaji wa kiuchumi na idadi ya vifo miongoni mwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.

Hali inatisha zaidi katika nchi za Afrika

Katika jamhuri ya Afrika kati hali inatajwa kuwa ni "mbaya sana"-Chad, Madagascar,Yemen na Zambia, hali ya njaa inatajwa kuwa ni "yenye kutisha sana".

Kwa jumla tangu mwaka 2000 juhudi za kupunguza balaa la njaa zimekuwa zikileta tija-balaa la njaa limepungua kuanzia wakati huo kwa kadiri asili mia 31. Kati ya nchi 119 zilizochunguzwa, 43 ndizo zilizoonyesha ishara ya kusumbuliwa na njaa.

Jukumu la mabadiliko ya tabianchi na madhara yake halijagawanywa  sawa sawa. Wale ambao sio wanaostahiki kulaumiwa sana kusababisha mabadiliko ya tabianchi ndio wanaoathirika zaidi-ameonya mwenyekiti wa shirika la Welthhungerhilfe Marlehn Thieme. Anakumbusha maafa yanayosababishwa na ukame, mafuriko na dhoruba. Shirika hilo linalopambana na njaa linashauri hatua maalum zichukuliwe kujikinga dhidi ya majanga pamoja na fedha za kutoshwa zitengwe kugharimia maafa ya mabadiliko ya tabianchi.

 

Mwandishi Jeppesen,Helle/Hamidou Oummilkheir

Mhariri: Iddi Ssessanga

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW