1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Port au Prince yazingirwa na magenge ya wahalifu

10 Machi 2024

Wakazi katika mji mkuu wa Haiti, Port au Prince wamelazimika kukimbilia mahali salama kufuatia mapigano baina ya magenge ya uhalifu.

Haiti yakumbwa na machafuko yanayotishia wakazi wa mji mkuu
Hali ni mbaya katika mji mkuu wa Haiti, Port au Prince wakati magenge ya wahalifu yakipambana na kuibua kitisho cha mji huo kuzingirwa na magenge hayoPicha: Odelyn Joseph/AP Photo/picture alliance

Mashambulizi haya yanafanyika wakati Umoja wa Mataifa ukionya juu ya mji huo kuzingirwa baada ya washambuliaji waliojihami kwa silaha kuyalenga makazi ya rais na makao makuu ya jeshi la polisi.

Siku ya Jumamosi, idadi kubwa ya wakazi walikimbilia kwenye majengo ya umma kujificha, ingawa ni baadhi tu ndio waliofanikiwa kuingia kwenye majengo hayo, hii ikiwa ni kulingana na shirika la habari la AFP.

Machafuko hayo yamesababisha Wahaiti 362,000 kuyakimbia makazi yao, na nusu kati yao wakiwa ni watoto na wengine wakilazimika kuhama zaidi ya mara moja, limesema Shirika la Kimataifa la Wahamiaji, IOM.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW