1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mji wa Hong Kong waendelea kukabiliwa na uchafuzi mkubwa wa hewa

Jason Nyakundi24 Aprili 2009

Hewa chafu yasababisha vifo vya mapema nchini china

Mji wa Hong Kong nchini China.Picha: picture-alliance / Helga Lade Fotoagentur GmbH, Ger

Uchafuzi wa hewa katika mji wa Hong kong umefikia viwango wa juu zaidi hata baada ya serikali ya china kufanya mikakati ya ya kukabiliana na hali hiyo. Uchafuzi wa hewa katika mji wa Hong Kong mara nyingi unasababishwa na kuongezeka kwa idadi ya viwanda hasa kusini mwa mpaka wa china.

Kutokana na utafiti uliofanywa hivi majuzi ulibainisha kuwa mmoja kati ya wakazi watano wa mji wa Hong Kong wanafikia kuuhama mji huo kutoka na kuchafuka kwa hewa. Kati ya watu 1000 waliohojiwa asilimia 97 walikuwa na wakazi wa kichina.

Michael DeGolyer proffesor wa masuala wa kisiasa aliyeendesha utafiti huo, alisema kuwa huenda wakati ukafika watu wakauhama mji huo wakiwemo mameneja pamoja na wasimamishi hasa wa makampuni.

Matokeo ya utafiti huo yanaashiria kuwa karibu watu milioni 1.4 wanamipango ya kuuhama mji wa Hong Kong wakiwemo watu nusu milioni ambao sasa hivi wamepanga kuondoka mji huo.

Kati ya wanaopanga kuhama ni watu wa kipato cha juu na waliopata masomo ya juu hali ambayo imezua hofu ya mji wa Hong Kong ulio kusini mwa china a kutowavutia watu walio na ujuzi wa juu.

Mwaka uliopita viwango nya uchafuzi wa hewa mjini Hong Kong vilipanda zaidi katika historia hata baada ya serikali kutangaza kuweka mikakati ili kuidhibiti hali hiyo.

Ripoti iliyotolewa mwaka uliopita ilionyesha kuwa takriban vifo 10,000 katika miji ya Hong Kong , Macau na eneo la kusini mwa china vinasababishwa na kuchafuka kwa hewa.

Moshi unaotoka kwenye viwanda kaskazini mwa nchi karibu na mji wa Hong Kong pamoja na ule unaotokana na shughuli mjini Hong Kong hasa viwandani na magari ulisababisha moshi huo kutanda katika anga za Hong Kong kwa muda mrefu mwaka uliopita.

Huku vumbi inayota kwa maelfu ya viwanda vya kila aina ikichangia kwa kiwango kikubwa katika mkoa wa Guangdong pia hewa chafu inayotoka kwenye vituo vya nishati vinayotumia makaa ya moto pamoja na malori mabovu vimechangia zaidi kwa uchafuzi wa hewa.

Wakati Teena Goulet alipohamia mji wa Hong Kong mwaka 1995 hakuwa na fikra kuwa siku moja atauhama mji huo lakini miaka mitano baadaye alijipata akiwa na kikohozi kikali. Baada ya kufanyiwa uchunguzi ilibainika kuwa alikuwa ameanza kuugua ugonjwa wa pumu na mwaka uliopita mwana uchumi huyo aliamua kuuhama mji wa Hong Hong.

Wiki moja tu baada ya kuwasili nyumbani Carlifonia nchini marekani kikohozi hicho kilitoweka.

Jim Rogers mwanabiashara wa kimarekani aliyehamia bara Asia mwaka 2007 pamoja na familia yake, akiamini kuwa china itakuwa kiungo muhimu cha kuimarika kwa uchumi wa dunia badala yake aliamua kuishi nchini Singapore kufuatia kuchafuka kwa hewa katika miji ya china.Alisema hataki hata kidogo kuvuta hewa ya Hong Kong.

Wanasayansi pamoja na wafanyabiashara wanaamini kuwa suala la kuchafuka kwa hewa linakuwa na hatari katika upande wa uchumi kwa kukosa kuwavutia wataalamu pamoja na wawekezaji.

Mji wa Shanghai nchini China.Picha: picture-alliance/ dpa

Sasa mataifa kama Australia yametoa tahadhari kwa raia wake kuwa hewa chafu katika mji wa Hong Kong inaweza kuchochea hali ya wagonjwa ambao bado wana maradhi ya kupumua kuwa mbaya zaidi

Pia wale wagonjwa walio na matatizo kama haya huwa wanashauriwa kukaa ndani mwa nyumba hasa wakati viwango vya uchafuzi wa hewa viko juu zaidi.

Sawia na nchini Bulgaria ambayo inatajwa kama nchi yenye hewa iliyochafuka zaidi barani ulaya, kulingana na ri jpoti iliyotolewa mapema mwaka huu hali ambayo ilitajiwa kuchangiwa zaidi na idadi kubwa ya magari mabovu pamoja na na idadi kubwa ya magari yaliyotumika yanayoingizwa nchini Bulgaria kutoka magharibi mwa Ulaya.

Katika mji wa Sofia ambayo ni makao ya mmoja kati ya kila WaBulgaria wanne viwango vya vumbi vimefikia kiwango cha juu zaidi.

Hata hivyo serikali ya china ijnasema kuwa imefanya juhudi za kupunguza kuchafuliwa kwa hewa katika mji wa Beijing kutokana na mikakati iliyowekwa wakati mji huo ulipoandaa mashindano ya olimpiki mwaka ulikopita.

China inahitajika kuchukua hatua zaidi na kuwa na sera zinazoleta mabadiliko ya kulinda uchafuzi wa hewa kwa mfano kuweka marufu kwa malorii mazito kuingia mitaani hasa wakati wa shughuli nyingi.

Hedley mwenye umri wa miaka 60 ameamua kuuhama mji wa Hong Kong baada ya kuishi katika mji huo kwa muda wa miaka 21.Hedley alichukua hatua hii baada ya kufanyiwa uchunguzi na kugundulika kuwa alikuwa akiugua maradhi ya Pumu.

Hata hivyo miji mingi katika bara la afrika inayoendea kupanuka kwa kasi huenda nayo ikakabiliwa na uchafuzi mkubwa wa hewa ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa mapema.

Mataifa mengi barani Afrika hayajaweka mikakati ya kuzuia uchafuzi wa hewa hata baada ya kubainika kuwa yako kwenye hatari ya kukabiliwa na viwango vya juu vya uchafuzi wa hewa.

Mara nyingi hali hii hutokana na ukosefu wa wataalamu wa kuweka sera mwafaka za kuzuia uchafuzi wa hewa, kutotengwa fedha za kufadhili shughuli hii kama vile kwenye miradi mingine.

Mwandishi: Jason Nyakundi/RTR

Mhariri: Mohammed AbdulRahman.






Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW