1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mji wa Kiev washambuliwa kwa droni

Josephat Charo
26 Novemba 2024

Idadi ya watu waliojeruhiwa kutokana na mashambulizi ya kutokea angani usiku wa kuamkia Jumatatu iliongezeka kufikia 23 katika mji wa Kharkiv, mashariki mwa Ukraine.

Vitali Klitschko, meya wa mji wa Kyiv
Vitali Klitschko, meya wa mji wa KyivPicha: DW

Meya wa mji wa Kyiv Vitali Klitschko amesema mji huo mkuu wa Ukraine umekabiliwa na shinikizo la mashambulizi ya droni usiku wa kuamkia leo.

Watu walioshuhudia wameliambia shirika la habari la Reuters kwamba wamesikia mfululizo wa milipuko katika kile kilichosikika kama mifumo ya ulinzi wa anga ikiwa kazini.

Mji wa Kyiv, eneo la viunga vyake na eneo kubwa la himaya ya Ukraine yamekuwa chini ya tahadhari ya kushambuliwa kutokea angani. Ving'ora vya kuwatahadharisha watu kuhusu mashambulizi ya kutokea angani vilianza kusikika tangu saa moja usiku hapo jana.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW