Mji wa Port Sudan washambuliwa kwa droni kwa siku ya sita
9 Mei 2025
Duru ya jeshi la Sudan imesema mashambulizi ya droni yameupiga mji wa bandari wa Port Sudan kwa siku ya sita mfululizo leo Ijumaa. Mshambulizi hayo ya masafa marefu yamdharibu miundombinu kadhaa muhimu, ukiwemo uwanja pekee wa ndege wa kimatiafa, ghala kubwa kabisa a mafuta na kituo cha umeme cha mji huo.
Duru hiyo ambayo haikutaka kutambulishwa, imewatuhumu wapiganaji wanamgambo wa kikosi cha Rapid Support Forces, RSF ambao wamekuwa wakipigana vita na jeshi la serikali tangu Aprili 2023.
Pia imesema mifumo ya ulinzi ya jeshi imezitungua baadhi ya droni za adui zilizolenga maeneo mbalimbali ya mji.
Watu walioshuhudia wameripoti mashambulizo katika maeneo ya Port Sudan, makao makuu ya serikali inayoungwa mkono na jeshi na kituo kikuu cha misaada nchini humo.