1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mjumbe wa Urusi arejea Marekani kwa mazungumzo ya Ukraine

31 Januari 2026

Mjumbe wa Urusi, kwa mazungumzo ya amani ya Ukraine, Kirill Dmitriev, amerejea nchini Marekani kuelekea duru nyingine ya mazungumzo ya amani kati ya Ukraine na Urusi yaliyopangwa kufanyika Jumapili huko Abu Dhabi.

Mjumbe wa Urusi Kirill Dmitriev akitembea baada ya mkutano na mjumbe wa Rais wa Marekani Donald Trump Steve Witkoff.
Mjumbe wa Urusi Kirill Dmitriev akitembea baada ya mkutano na mjumbe wa Rais wa Marekani Donald Trump Steve Witkoff.Picha: Alexei Alekseyev/SNAIMAGO

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mjumbe huyo ameandika amerejea Miami, bila ya maelezo ya kina na kuweka alama ya njiwa wa amani. Katika mikutano ya awali, Dmitriev amekuwa akijadiliana na mjumbe wa Marekani, Steve Witkoff. Mazungumzo hayo mjini Abu Dhabi, ambayo yalianza tena wiki iliyopita baada ya kusimama kwa muda mrefu, yanakusudia kuchunguza uwezekano wa kupatikana njia ya kumaliza vita vya Ukraine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW