1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Mjumbe wa Marekani aonya dhidi ya vita mpakani mwa Lebanon

4 Machi 2024

Mjumbe maalum wa Marekani Amosi Hochstein, amesema hata vita vya kiwango cha chini kwenye mpaka wa kaskazini mwa Lebanon havitaweza kudhibitiwa.

Mpaka kati ya Israel na Lebanon
Mzozo umekuwa ukiongezeka kati ya Israel na Hezbollah tangu kuanza kwa uvamizi wa Gaza.Picha: Taher Abu Hamdan/Xinhua/picture alliance

Mjumbe maalum wa Marekani Amosi Hochstein, amesema hata vita vya kiwango cha chini kwenye mpaka wa kaskazini mwa Lebanon havitaweza kudhibitiwa.

Mjumbe huyo anafanya ziara ya siku moja nchini Lebanon katika juhudi za kuepusha uhasama kati ya Hezbollah na Israel kugeuka kuwa vita kamili.

Soma pia: Borell aonya Lebanon kuingizwa vitani Mashariki ya Kati

Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran wamekuwa wanakabiliana na Israel kwa miezi kadhaa wakati ambapo vita katika Ukanda wa Gaza vinapoendelea.

Makabaliano hayo ni mgogoro mkubwa kuwahi kutokea katika eneo la kusini mwa Lebanon tangu vita vya mwaka 2006. Mgogoro huo unaochochea hofu ya kuzuka vita kubwa zaidi.