1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mjumbe wa Marekani kuhusu Mashariki ya Kati yuko Beirut

19 Novemba 2024

Mjumbe wa Marekani kuhusu Mashariki ya Kati Amos Hochstein, amewasili mjini Beirut katika juhudi za kukamilisha makubaliano ya kusitisha vita kati ya Israel na kundi la Hezbollah la nchini Lebanon.

Libanon Amos Hochstein - Senior Advisor U.S. Präsident Joe Biden
Mshauri Mkuu wa Rais wa Marekani Joe Biden Amos Hochstein, akionyesha ishara alipokutana na Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati, mjini Beirut, 14.11,2024. Picha: Hussein Malla/AP Photo/picture alliance

Kwa mujibu wa chanzo cha serikali, mjumbe huyo wa Marekani atakutana leo mchana na spika wa bunge Nabih Berri anayeliwakilisha kundi la Hezbollah katika mazungumzo hayo. Ziara ya Hochstein, Lebanon, inafanyika katika wakati ambapo jeshi la Israel limeripoti leo Jumanne, kwamba kiasi maroketi 40 yamefyetuliwa kutoka Lebanonkuelekea kaskazini na katikati mwa Israel na kusababisha watu wanne kujeruhiwa na vigae vya madirisha ya jengo lililolengwa na maroketi hayo. Jeshi la Israel pia limesema kundi la wanamgambo la Hezbollah ambalo linaungwa mkono na Iran, limefanya mashambulio hayo wakati kikosi cha wanaanga cha nchi hiyo kikiendesha mashambulizi makubwa dhidi ya mji wa Beirut, jana Jumatatu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW