1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani: Sudan ni mgogoro mkubwa zaidi wa kiutu duniani

17 Novemba 2025

Mjumbe wa Rais wa Marekani Donald Trump, kwa Afrika Massad Boulos, amesema vita vya Sudan ni "mgogoro mkubwa zaidi wa kibinadamu duniani”, na kuwa anatarajia kuona maendeleo ya kidiplomasia kuelekea amani.

Mjumbe Maalum wa Marekani Massad Boulos katika mkutano na waandishi wa habari kufuatia makubaliano ya kusitisha mapigano
Mjumbe Maalum wa Marekani Massad Boulos katika mkutano na waandishi wa habari kufuatia makubaliano ya kusitisha mapiganoPicha: Karim Jaafar/AFP

Akizungumza na Shirika la Habari la Ufaransa AFP, mjini Doha amesema "Hasa kilichotokea El-Fasher katika wiki mbili au tatu zilizopita. Sote tumeona video hizo. Tumeona ripoti hizo. Ukatili huo haukubaliki kabisa.

Hili lazima likome haraka sana.”Tangu kuzuka mapigano Aprili 2023, kati ya jeshi la Sudan na wapiganaji wa RSF kumetokea vifo vya makumi ya maelfu ya watu na kuwapotezea makazi karibu watu milioni 12.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW