1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLibya

Mjumbe wa UN asema uthabiti wa Libya umo mashakani

23 Agosti 2023

Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Libya, Abdoulaye Bathily, amesema uthabiti wa taifa hilo umo mashakani baada ya kuzuka mapigano kati ya makundi hasimu mjini Tripoli hivi karibuni.

Libyen | Mapigano Tripoli
Libya imetumbukia kwenye machafuko tangu kuangushwa utawala wa Muammar Ghaddaffi mwaka 2011Picha: Yousef Murad/AP/picture alliance

Mwanadiplomasia huyo ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba migawanyiko ya kisiasa nchini Libya inabeba kitisho cha kutokea machafuko na mparaganyiko kwa taifa kama ilivyoshuhudiwa kwenye mataifa mengine duniani.

Amezirai pande hasimu nchini humo kumaliza tofauti zao juu ya suala la kufanyika uchaguzi akisema zoezi hilo la kidemokrasia linabeba matumaini makubwa ya kurejea kwa uthabiti nchini Libya.

Bathily ametahadharisha kwamba bila makubaliano jumuishi ya kisiasa yatakayofanikisha uchaguzi huru na wa uwazi, hali nchini Libya itazidi kuzorota na kupalilia madhila kwa umma wa taifa hilo.