Mjumbe wa UN kwa Libya: Uchaguzi unawezekana
17 Oktoba 2023Matangazo
Mkwamo kati ya pande hasimu za kisiasa na makundi ya waasi kuhusu serikali ya mpito umeshuhudiwa tangu mapema mwaka uliopita, hali ambayo imeibua mapigano ya mara kwa mara.
Soma zaidi: Mjumbe wa UN asema uthabiti wa Libya umo mashakani
Bathilya alikwa akizungumza mbele ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa baad ya spika wa bunge la Libya mashariki kutangaza sheria mpya za uchaguzi kwa kuzingatia muongozo wa diplomasia ya kimatiafa unaolenga kuutanzua mgogoro wa miaka mingi kupitia uchaguzi.
Soma zaidi: Umoja wa Mataifa waonya kuhusu machafuko Libya
Bathily amesema uchaguzi wa Libya unahitaji serikali imara yenye umoja itakayokubaliwa na wadau wakuu wa mashariki na magharibi ambao kufikia sasa wameonesha ari ndogo kuafikiana.