1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkakati wa China kudhibiti idadi ya watu wa Xinjiang

24 Mei 2021

China siyo tu inalaumiwa ukandamizaji dhidi ya jamii ya Waislamu wachache wa Uyghurs, bali imekwenda mbali zaidi kwa kuwalazimisha wanawake wa jamii za wachache kufunga vizazi kwa lengo la kudhibiti idadi yao.

Bildreihe DPA China Xinjiang Flash Format
Picha: picture-alliance / dpa/dpaweb

Mwaka 2019 Qelbinur Sedik alikuwa na umri ambao siyo rahisi kwa mwanamke kubeba mimba lakini anasema mamlaka za China zilimlazimisha kufunga kizazi katika kile anachokitaja kuwa kampeni pana ya serikali mjini Beijing ya kupunguza uzazi kwenye jamii ya Uyghurs na jamii nyingine za wachache katika jimbo tete la Xinjiang.

Ukimya wa nchi jirani na China kuhusu mateso dhidi ya jamii ya Uighur

This browser does not support the audio element.

Akiwa na umri wa miaka 50 mwanamama huyo alizisihi mamlaka kutomlazimisha kuwekewa kijiti kinachotumika kuzuia mimba kwa sababu mara kadhaa njia hiyo ilimsababishia maumivu makali na kutokwa na damu.

Hakuna aliyemsikiliza, alilazimishwa kufunga kizazi katika kliniki moja iliyopo kwenye mji anakotoka wa Urumqi huku akitishwa kuwa angechukuliwa hatu iwapo angekataa.

Soma pia:Maelfu ya Wauighur wanafanyishwa kazi kwa lazima

Anasimulia kuwa aliporejea nyumbani alivuja damu mfululizo kwa siku kadhaa na hadi leo bado anaandamwa na maumizi yalisiyokwisha na kuvuja damu katika hali isiyo ya kawaida.

Wanawake wa jamii ya Waislamu wa Uyghur wakiwa kwenye mtaa wa manunuzi katika mji wa Kashgar, Xianjiang, China.Picha: Imago-Images/alimdi

Mwanamke huyo kutoka kabila la Uzbek, moja ya jamii za waislamu wachache wanaoishi katika jimbo la Xinjiang hukoChina, hivi sasa anatafuta hifadhi nchini Uholanzi.

Kwenyejimbo la Xianjing takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha uzazi kiliporomoka kwa karibu asilimia 50 kati ya mwaka 2017 hadi 2019, kiwango amabcho ni cha chini zaidi kuwahi kurikodiwa duniani tangu mwaka 1950.

Kwa miongo mingi, Xianjiang imekuwa na kiwango cha juu cha uzazi kuliko majimbo yote ya China hali iliyoongeza idadi yajamii ya Uyghurs. Hivi leo jimbo hilo ni makaazi ya waislamu milioni 12, idadi ambayo ni karibu nusu ya wakaazi wote wa jimbo hilo.

Lakini sasa ongezeko la idadi ya watu limeporomoka hadi kiwango sifuri na kwenye maeneo mengine hakuna kabisa watoto wanaozaliwa.

Soma pia: China yashtumiwa kuwapangisha uzazi kwa lazima Waiughur

Ripoti ya mwaka 2020 iliyotolewa na serikali ya China inaonesha matumizi ya njia za kuzuia watu kupata mimba yalipanda kutoka 3,214 mwaka 2014 hadi 60,000 mwaka 2018 huku jimbo hilo likiwa na asilimia 80 ya njia za kufunga uzazi zilzotumika nchi nzima kwa mwaka huo wa 2018.

Shinikizo kwa jamii za wachache

Ingawa China inafahamika kwa utekelezaji wa sera ya kuzuia uzazi, lakini kwa sehemu kubwa shinikizo linawekwa zaidi kwa jamii za wachache ikilenga kupunguza idadi yao duniani.

Waandamanaji wa kundi la kikabila la Uyghur katika mkoa wa Xinjiang wakiandama nje ya ikulu ya Marekani, White House kupinga ukandamizaji wa serikali ya China dhidi ya jamii yao.Picha: Michael Reynolds/dpapicture-alliance

"Kupunguza ongezeko la idadi ya watu huko Xianjing kunakwenda sambamba na malengo ya chama cha kikomunisti cha China kwenye mkoa huo" anasema Adrian Zenz, msomi katika wakfu wa kumbukumbu za wahanga wa ukomunisti mjini Washington.

Hata hivyo mara kadhaa China imesma msomi huyo amekuwa akipotosha taarifa zake kwa kueneza uzushi dhidi ya taifa hilo.

Lakini siyo Zenz pekee anayetizama sera hizo za China kwa jicho la tahadhari. wasomi na watetezi wengi wa haki za binadamu wamekuwa wakisema sera za China za tangu mwaka 2017 za kudhibiti kiwango cha uzazi -ikiwemo kulazimisha wanawake kufunga kizazi na kuwapeleka jela watu wenye watoto wengi - ni sehemu ya hatua za makusudi za kujaribu kupunguza idadi ya watoto wanaozaliwa kwenye jamii za walio wachache huko Xinjiang.

Soma pia: Namna China inavyowafunga Wauighur bila sababu za msingi

Sera hizo zinakwenda sambamba na kampeni ya kuanzisha kambi za kubadilisha watu imani amabko mamilioni wa Uyghurs na watu wa jamii nyingine za wachache wamekuwa wakipelekwa kwa madai kuwa seirkali inalenga kukabiliana na itikadi kali ya kiislamu inayohushishwa na matendo ya uhalifu kwenye jimbo la Xinjiang.

Mataifa mengi ya magharibi yamezitaja hatua hizo za China kuwa zenye leo la kuangamiza jamii za wachache, madai ambayo yanaungwa mkono na watetezi wengi wa haki za binadamu.

Chanzo: AFP

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW