1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkanganyiko kwenye mkutano wa tatu baina ya waislamu na serikali ya Ujerumani

Abdu Said Mtullya30 Machi 2011

Utatanishi wajitokeza kwenye mkutano baina ya Waislamu na serikali ya Ujerumani

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Hans-Peter Friedrich(kati kati)kwenye mkutano wa BerlinPicha: dapd

Viongozi wa dini ya kiislamu wamekutana na wawakilishi wa serikali ya Ujerummani mjini Berlin kwenye mkutano wa tatu uliopaswa kujadili njia za kuundeleza mchakato wa kuwaingiza waislamu katika jamii ya Ujerumani.

Lakini waziri mpya wa mambo ya ndani Hans Peter Friedrich aliitumia fursa ya mkutano huo kuzungumzia masuala ya usalama.

Waziri huyo mpya wa aliekuwa mwenyekiti wa mkutano huo kwa mara ya kwanza aliwaambia viongozi wa dini ya kiislamu kwamba serikali ya Ujerumani inataka kuwepo ushirika wa kiusalama na waislamu zaidi ya milioni nne wanaoishi nchini.Waziri Friedrich alisema kwenye mkutano huo mjini Berlin kwamba serikali ya Ujerumani inadhamiria kushirikiana na waislamu ili kuzuia hatari ya itikadi kali na siasa kali.

Lakini madhumuni ya mkutano huo wa tatu, sawa na ile iliyokwishafanyika lilikuwa kujadili njia za kuuendeleza mchako wa kuwashirikisha waislamu zaidi ya milioni na jamii ya Ujerumani.

Kabla ya mkutano huyo kufanyika tayari mambo yalienda mrama baada ya Waziri mpya Hans -Peter Friedrich kusema kwamba hakuna ushahidi wa kihistoria unaoonyesha kwamba Uislamu ni sehemu ya utamaduni wa Ujerumani. Ingawa amekiri kwamba wapo waislamu wanaoishi nchini Ujerumani. Amesema ni wazi kwamba waislamu wengi wanaoishi nchini ni sehemu ya jamii.

Hata hivyo waziri huyo ameeleza kuwa pana suala la utambulisho wa utamaduni wa kijerumani.Amesema Ujerumani ni jamii yenye nasaba ya Ukristo.

Lakini licha ya kusema kuwa waislamu ni sehemu ya jamii na kutoa mwito kuwata waislamu hao wajishirikishe na jamii,viongozi wa dini ya kiislamu waliohuduria mkutano wa mjini Berlin wamesema kuwa kauli hiyo haitoshi.

Mwakilishi wa shirikisho la Misikiti ya Ujerumani, DITIB Bekir Alboga amesema kuwa kauli ya waziri Friedrich kwamba, waislamu ni sehemu ya Ujerumani lakini Uislamu siyo sehemu ya Ujeruman ni hatua ya kuchochea chuki dhidi ya Uislamu.

Akijibu mwito wa waziri Friedrich juu ya kujenga ushirikiano wa usalama baina ya serikali ya waislamu,mtaalamu wa Uislamu Armina Omerika amesema hatua hizo za usalama zitahamasisha utaratibu wa mashaka wa kuwapeleleza waislamu wengine."Utaratibu huo hautahimiza mchakato wa kuwaingiza waislamu katika jamii"

Baraza Kuu la Waislamu la Ujerumani lilijiondoa kwenye mikutano hiyo mwaka uliopita ,kama ishara ya kupinga mikutano hiyo kutumiwa kama jukwaa la kujadili masuala ya usalama.

Hata hivyo waziri wa elimu wa Ujerumani bibi Annette Schavan amearifu kuwa vitengo vya mafunzo ya dini ya kiislamu vitaanzishwa kwenye vyuo vikuu vinne vya Ujerumani.

Mwandishi/Sabine Ripperger/

Tafsiri/Mtullya abdu/

Mhariri/ Abdul - Rahman

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW