1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkanyagano kwenye uwanja wa soka wauwa 12 El Salvador

21 Mei 2023

Watu 12 wamepoteza maisha jana Jumamosi baada ya kutokea mkanyagano katika uwanja wa mpira huko El Salvador ambapo mashabiki wa soka walikuwa wamekusanyika kutazama mchuano wa ndani wa kandanda.

 El Salvador, San Salvador | Massenpanik im Fussballstadion
Picha: Milton Flores/AP/dpa/picture alliance

Ripoti za awali za kimamlaka zilionesha kuzuka kwa vurugu baada ya mashabiki wa soka kutaka kuingia katikati ya uwanja wa Cuscatlan wakati wa mechi kati ya timu za Alianza na FAS.

Msemaji wa timu ya usaidizi wa dharura ya Comandos de Salvamento, Carlos Fuentes alisema kufuatia mkasa huo wamekuwa wakiwapa matibabu zaidi ya watu 500. Watu 100 kati ya hao wako katika hali mbaya zaidi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW