1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaYemen

Mkanyagano Yemen wakati wa kutolewa msaada wauwa watu 85

20 Aprili 2023

Zaidi ya watu 85 wamekufa na mamia ya wengine kujeruhiwa katika mkanyagano kwenye hafla ya usambazaji wa misaada katika taifa lililoharibiwa kwa vita la Yemen.

Hilo ni moja kati ya matukio mabaya zaidi ya mkanyaganao kuwahi kutokea nchini humo katika muongo mmoja. Tukio hilo limetokea ikiwa imesalia siku moja tu kabla ya Siku Kuu ya Eid al-Fitr, ambayo inaadhimisha mwisho wa mwezi mtukufu wa Kiislamu wa Ramadhan.

Afisa wa usalama wa serikali ya Wahouthi amesema mkanyagano huo uliotokea katika kitongoji cha Bab al-Yemen cha mji mkuu Sanaa. Kila mmoja alikuwa anapokea dola nane. Kwa mujibu ya walioshuhudia ni kwamba mamia ya watu walikusanyika kwenye shule moja kwa ajili ya kupata msaada uliokuwa unatolewa na wafanyabiashara wawili ambao tayari wamekamatwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW