Mkataba wa biashara huru baina ya Umoja wa Ulaya na Africa wazua tetesi
9 Mei 2007Mwaka 2000,Umoja wa Ulaya na wanachama 79 wa mataifa ya ACP Africa Caribean na Pacific walikubaliana kutathmini kikamilifu atahri zinazoweza kutokea kutokana na makubaliano ya mapendekezo ya ushirikiano wa biashara huru na Umoja wa Ulaya, EPA. Maamuzi haya yaliafikiwa na wajumbe wa serikali zilizokutana Cotonou katika mji mkuu wa Benini.
Lakini ziara ya Katibu mkuu wa mataifa wanachama wa ACP,John Kaputin iliyofanwa kwa kimya kingi Afrika kusini ilizua wasiwasi kuhusu mazungumzo ya mkataba huo. Kaputin alifanya mazungumzo na waziri wa mambo ya kigeni wa Afrika Kusini Nkosazana Dlamini-Zuma na wawakilishi wa wizara ya biashara na viwanda. Alikutana pia na spika wa bunge la Umoja wa Africa,Getrude Mongella na katibu mkuu wa NEPAD Olukorede Willoughby.
Lakini yaliozungumziwa katika mkutano huu hayakuelezewa kwa kina na hata wadau na wanaharakati wa kulinda haki za kibiashara za Africa hawakufahamishwa juu ya mikutano hii.
Mwanaharakati mmoja wa kituo cha Mawasiliano na maendeleo Cape Town Dot Keet, hawataruhusu mazungumzo yeyote kuendelea baina ya mataifa hayo na Umoja wa Ulaya hadi utathmini wa mapendekezo yao utakapofanywa.
Mazungumzo ya kupitisha mkataba mpya wa ushirikiano huru wa kibiashara na Umoja huo yalianza mwaka 2002 kwa madhumuni ya kuondoa mkataba wa nafuu wa kibiashara ilioundwa miaka thelathini iliyopita. Wanaharakati hawa wanasema tetesi yao ni kwamba maazimio ya mikataba hii mipya haijulikani na jinsi yatavyoathiri mataifa ya Afrika Caribic na Pacific.
Vongozi wa makanisa ya Afrika kusini na Mashariki walisema, wanashkuru kua mataifa haya yanafanya majadiliano ya ushirika wa kiuchumi lakini makubaliano haya yatalinda uhai wetu kiuchumi? Kwani makubaliano haya mapya yanaonekana kuimarisha biashara bila vikwazo vyevyote kwa mataifa ya Umoja wa ulaya na huenda yakaathiri sekta ya kilimo,viwanda rasilmali na nishati za mataifa maskini.
Kulingana na kundi la wanaharakati wa Uingereza wanaotetea maswala ya Africa,walisema huenda Guinea Bissau na Cape Verde wakapoteza asili mia kumi na tisa ya mapato yao.
Na Ghana huenda wakapoteza dolla millioni 194 ya mapato yake pia kutokana na mkataba huo wa biashara uhuru.
Makanisa pamoja na wanaharakati wa Afrika wametoa wito kuongezwa kwa tarehe ya mwisho ya mazungumzo ya Umoja wa Ulaya na ACP kutoka tarehe 31 mwezi Desemba. Hatua hii itawezesha serikali za mataifa maskini kulainisha maazimio yanayonekana kuzorotesha uchumi wake.
Richard Kamidza wa kituo cha kutatua mizozo ACCORD,kilichoko Durba Afrika kusini,alisema lazima maswala haya yaelezwe kwa uwazi kwa serikali na wadau. Kwani ikiwa Umoja wa Ulaya unaweza kuchukua mwaka kujadili uwezo wa Afrika Kusini kujumuishwa katika mataifa wanachama ya ACP,basi pia wanaweza kuongeza muda wa majadiliano haya ya ushirika wa biashara huru.
Wanaharakati hawa wamesema Umoja wa Ulaya unaharibu umoja wa mataifa ya ACP kwa kushinikiza ajenda zake. Istoshe Umoja wa Ulaya sio nguvu pekee ya kiuchumi inayowania nafasi ya kibiashara barani Africa,China nayo iko tayari kuwekeza zaidi katika eneo hilo.
Mashirika hayo ya kiraia yametoa wito kwa Katibu mkuu wa mataifa hayo ya ACP kuweka juhudi zao katika kutekeleza ahadi za mataifa tajiri kuendeleza bara hili la Africa kwani ahadi nyingi hazijatekelezwa.
Isabella Mwagodi.