Mkataba wa kijeshi wa Urusi, Korea Kaskazini waanza kazi
5 Desemba 2024Taarifa iliyotolewa na shirika hilo hivi leo inasema mkataba huo umeanza kazi baada ya Moscow na Pyongyang kukabidhiana nyaraka za kuidhinishwa hapo jana.
Mkataba huo unauweka ushirikiano wa kijeshi baina ya mataifa hayo mawili kwenye ngazi ya juu zaidi, na unaelezea kwamba zitasaidiana pale mmoja wao anaposhambuliwa.
Soma zaidi: Korea Kaskazini yaahidi kuendelea kuisaidia Urusi katika vita dhidi ya Ukraine
Waziri wa Ulinzi wa Urusi, Andrey Belousov, amesema ushirikiano huo unadhamiria kupunguza hatari ya vita kwenye eneo la kaskazini mashariki mwa Asia.
Mkataba huo unaanza kazi wakati tayari Korea Kaskazini imetuma maelfu ya wanajeshi nchini Urusi kuisaidia kwenye vita vyake dhidi ya Ukraine, kwa mujibu wa duru za kijasusi za mataifa ya Magharibi.