Mkataba wa Mercosur wapelekwa mahakamani
21 Januari 2026
Bunge la Ulaya limepitisha uamuzi wa kuupeleka mkataba unaozozaniwa wa biashara huria unaofahamika kama Mercosur, kati ya Umoja wa Ulaya na mataifa manne ya Amerika ya Kusini, mbele ya mahakama ya haki ya Ulaya ECJ kutathminiwa.
Wabunge 334 wameunga mkono hatua ya mkataba huo kupelekwa ECJ kufanyiwa tathmini ya kisheria huku wabunge 324 wakipinga na 11 walijizuia kupiga kura katika mchakato uliofanyika hivi leo mjini Strassbourg.
Nchi za EU zaridhia mkataba wa biashara huru Mercosur
Kupelekwa mbele ya mahakama ya ECJ mkataba huo wa kibiashara unaofahamika kama Mercosur, huenda kukachelewesha kuidhinishwa na mataifa ya Brazil, Argentina, Paraguay na Uruaguay.
Mkataba wa biashara wa EU-Mercosur wasogezwa mbele kufuatia ombi la Italia
Nchi za Umoja wa Ulaya zinazoupinga mkataba huo zinataka mabunge ya nchi za Jumuiya hiyo pia zipewe mamlaka ya kuuidhinisha, badala ya jukumu hilo kuachiwa bunge la Ulaya peke yake.