1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Marekani yahujumu mkataba wa hali ya hewa

Josephat Charo
5 Mei 2025

Marekani inapania kudhoofisha mkataba wa kimataifa unaonuiwa kuzisaidia nchi zinazoendelea zinazopambana kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na masuala mengine. Hayo ni kwa mujibu wa Umoja wa Matiafa.

Umoja wa Mataifa
Viunga vya Umoja wa MataifaPicha: Hauke-Christian Dittrich/picture alliance

Umoja wa Mataifa unatafuta mpango wa maendeleo endelevu kabla mwezi Juni mwaka huu. 

Utawala wa Trump unapinga rasimu ya mageuzi ya mfumo wa fedha wa dunia yanayonuiwa kuzisaidia nchi zinazoendelea, yakiwemo kuhusu utozaji kodi, viwango vya riba kwa mikopo na ruzuku ya nishati inayopatikana chini ya ardhi. Pia utawala huo unataka masuala ya hali ya hewa, usawa wa kijinsia na maendeleo endelevu yafutwe katika rasimu hiyo.

Hati hiyo ambayo haijawahi kuripotiwa unatoa maelezo kuhusu jinsi utawala wa Trump unavyotaka kushinikiza ajenda ya Marekani Kwanza, zikiwemo juhudi za kupunguza kasi ya mabadiliko ya hali ya hewa na kuendeleza utofauti katika taasisi ambazo ziko katika shina la kushughulikia mizozo ya kimfumo ya kimataifa.

Mkutano wa nne wa kimataifa kuhusu Fedha na Maendeleo, unaofanyika mara moja katika muongo mmoja, ambao umepangwa kufanyika mwezi Juni mjini Seville nchini Uhispania, unalenga kushawishi muelekeo wa kimkakati wa maendeleo ya taasisi za fedha za dunia.

Athari za mafuriko na kimbunga kusini mwa Tanzania

05:58

This browser does not support the video element.

Soma pia:Maandamano ya Uturuki yalenga kudhibiti madaraka ya Erdogan

Nchi zilikubaliana kwa mfano katika katika mkutano wa tatu uliopita, kutanua ushrikiano katika masuala ya kodi ili nchi zinazoendelea ziweze kusaidia kuweka sheria na taratibu na hadi kufikia Mei mwaka uliopita, zaidi ya nchi 140 zilikuwa zimeshirikishwa.

Tom Mitchell, mkurugenzi mkuu wa taasisi ya kimataifa ya mazingira na maendeleo ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba mkutano wa mwezi Juni unalenga kuwaleta pamoja viongozi wa dunia na kuweka sheria za msingi na vipaumbele kwa ajili ya malengo ya maendeleo ya kifedha katika kipindi cha muongo mmoja ujao.

Hati hiyo iliyoandaliwa na wawakilishi wa kudumu katika Umoja wa Mataifa kutoka Mexico, Nepal, Norway, na Zambia kwa msaada wa sekretariati ya Umoja wa Mataifa, rasimu ya Aprili 11 inajumuisha maelezo ya misimamo ya nchi 193 zilizoshirikishwa katika mashaurino hayo.

Jitihada za mageuzi kudhoofishwa

Mabadiliko yanayoendelea katika Benki ya Dunia na Fuko la Fedha la Kimataifa katika kupambana na madiliko ya hali ya hewa yakikabiliwa na upinzani kutoka kwa waziri wa fedha wa Marekani Scott Bessent, hati hiyo inaonesha wizara hiyo inapanga kudhoofisha jitihada zaidi za mageuzi.

Miongoni mwa vipengee maalumu katika hati vinavyohusu mageuzi ya kimfumo, hati hiyo inaonesha kwamba Marekani inataka kuondosha maneno yanayotaja mkusanyiko wa mageuzi kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Athari za mabadiliko ya hali ya hewa Afrika

01:41

This browser does not support the video element.

Badala yake inataka kuondoa sentensi inayoahidi kuufanyia mageuzi muundo wa kimataifa wa fedha na kuweka maneno ya kuahidi kutambua umuhimu wa kuimarisha uthabiti na ufanisi wake katika kukabiliana na changamoto na majanga ya sasa na yajayo.

Mabadiliko kama haya katika lugha yanaashiria kiwango cha pamoja cha ahadi ambayo inaweza kutumika kama msaada kwa kuchukua hatua au kutochukua hatua katika mazungumzo ya siku za usoni.

Soma pia:Taliban yakataa waranti wa ICC ikisema 'imechochewa kisiasa'

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amekiri anatambua haja ya kuzishinda changamoto nyingi kabla ya mkutano wa Juni, lakini akahimiza nchi zote kuwa katika meza ya mazungumzo mjini Sevilla wakielekeza nguvu katika kutafuta suluhu, kama alivyosema msemaji wake Florencia Soto Niño katika barua pepe kwa shirika la habari la Reuters.

Ikulu ya Marekani na wizara ya fedha hawakujibu maombi ya kuwataka watoe maelezo. Wizara ya mambo ya nje ilikataa kutoa kauli.

Wakati msimamo wa Marekani kuhusu maendeleo ukiwa umezidi kuwa mgumu chini ya Trump, hati ya mazungumzo inaonyesha nchi hiyo bado inaunga mkono juhudi zinazojumuisha nchi zinazoendelea kufanya kazi kwa karibu zaidi na sekta binafsi, na kukuza uvumbuzi na ujuzi wa kifedha.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW