1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mke wa Dedan Kimathi afariki dunia

5 Mei 2023

Mjane wa kiongozi la wapiganaji wa Mau Mau lililoongoza vita vya silaha dhidi ya ukoloni wa Muingereza nchini Kenya, Dedan Kimathi, amefariki dunia.

Kenia Nairobo 2013 | Wandgemälde, Friedensbotschaft
Picha: Phil Moore/AFP/Getty Images

Mukami Kimathi aliyekuwa na umri wa miaka 101 amefariki katika hospitali ya Nairobi usiku wa kuamkia Ijumaa (Mei 5).

Kulingana na binti yake, Everlyne, aliyenukuliwa na vyombo vya habari, Mama Mukami alikimbizwa hospitalini siku ya Alhamis (Mei 4) alipopatwa na matatizo ya kupumua.

Kabla ya kifo chake, mjane huyo alikuwa akiishinikiza serikali kufukua mabaki ya maiti ya marehemu mume wake kutoka jela yenye ulinzi mkali ya Kamiti ili azikwe kwake.

Dedan Kimathi: shujaa wa uhuru wa Kenya

02:08

This browser does not support the video element.

Kauli hizo zimepewa uhai mpya hii leo baada ya Waziri wa Biashara na Viwanda, Moses Kuria, kulitilia mkazo hilo kwenye ujumbe wake wa pole kwa familia.

Wakati huo huo, Rais William Ruto na naibu wake, Rigathi Gachagua, wametuma salamu za rambirambi kwa familia na kuahidi kumfanyia maziko ya hadhi ya juu.

Duru rasmi zinaeleza kuwa Dedan Kimathi alikamatwa na utawala wa ukoloni mwaka 1956 katika eneo la Kahigaini iliko milima ya Aberdares, na kuuawa mwaka 1957 kwenye gereza la Kamiti.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW