Mke wa mgombea urais alipwa euro 600,000
25 Januari 2017Kwa mujibu wa gazeti la dhihaka liitwalo Le Canard Enchaine, Penelope Fillon alikuwa akilipwa fedha hizo kwa kazi ya kuwa msaidizi wa masuala wa kibunge ya mumewe na baadaye kama naibu kwenye bunge la taifa na kisha kwenye kazi katika jarida moja la mambo ya kitamaduni.
Hata hivyo, gazeti la Le Canard Enchaine linasema hakuna ushahidi ikiwa mwanamke huyo aliwahi kufanya kazi yoyote kati ya hizo ambazo alikuwa akilipwa mishahara.
Mwenyewe Fillon amesema hivi leo (Jumatano, Januari 25) kwamba amekasirishwa sana na ripoti hiyo ambayo ameiita ya "uchochezi na upotoshaji".
"Nimekasirishwa na uchafuaji huu na uzushi wa makala hii," alisema Fillon, ambaye ni waziri mkuu wa zamani wa Ufaransa akiwa upande wa wahafidhina na ambaye sasa anawasia urais kwa tiketi cha chama Republican kwa uchaguzi utakaofanyika tarehe 23 Aprili na 7 Mei mwaka huu.
Mwandishi: Mohammed Khelef/Reuters
Mhariri: Josephat Charo