1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUganda

Mke wa mwanasiasa Besigye asema mumewe ametekwa nyara

20 Novemba 2024

Mke wa mwanasiasa kinara wa upinzani nchini Uganda Kiza Besigye amesema mumewe anashikiliwa kwenye jela moja ya kijeshi baada ya kukamatwa kwa nguvu nchini Kenya.

Kinara wa upinzani nchini Uganda Kiza Besigye
Kinara wa upinzani nchini Uganda Kiza BesigyePicha: Ben Curtis/AP/picture alliance

Mke wa mwanasiasa kinara wa upinzani nchini Uganda Kiza Besigye amesema mumewe anashikiliwa kwenye jela moja ya kijeshi baada ya kukamatwa kwa nguvu nchini Kenya.

Winnie Byanyima, mke wa Besigye na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Ukimwi, UNAIDS, ametoa taarifa hizo leo kupitia mtandao wa kijamii wa X na kuitaka serikali ya Uganda kumwachia "mumewe haraka kutoka eneo lolote inakomshikilia."

Soma pia: ICC kuthibitisha mashitaka dhidi ya mbabe wa kivita Kony

Kulingana na Byanyima, mwanasiasa huyo alitekwa nyara Jumamosi iliyopita mjini Nairobi alikokwenda kuhudhuria halfa ya uzinduzi wa kitabu cha mwanasiasa wa upinzani wa nchi hiyo Martha Karua. Amesema anazo taarifa za uhakika kwamba Besigye anashikiliwa hivi sasa kwenye jela moja mjini Kampala.

Mamlaka za Uganda zimesema zinachunguza madai hayo ya kutoweka kwa Besigye zimekuwa zikifanya ukandamizaji mkubwa dhidi ya upinzani miezi ya karibuni ikiwa ni pamoja na kuwakamata viongozi vigogo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW