1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkesha wa Krismas Bethlehem

24 Desemba 2010

Leo ni mkesha wa sikukuu ya Krismas, ambayo inaadhimishwa kote duniani, kesho tarehe 25

Askofu wa Mashariki ya Kati Fouad Twal(kati) leo ataongoza misa ya mkesha wa krismasPicha: AP

Huko Bethelem alikozaliwa Yesu Masia, maelfu ya watu kutoka kote duniani wamekuwa wakimiminika, wakiwemo kwa mara ya kwanza wakristo kutoka mataifa ya kiarabu yasiyokuwa na uhusiano wa kidiplomasia na Israel.

Tokea mapema leo asubuhi, mitaa ya mji huo wa Bethlehem uliyoko katika ukingo wa magharibi, imepambwa kwa miti na taa za Krismas.

Vijana wa kipalestina wakiwa wamevaa nguo za rangi ya bluu isiyo kooza wanajiandaa kwa mkesha huo, huku bendi ikifanya mazoezi na nyimbo za Krismas zikisikika kutoka katika maduka.

Polisi wa Mamlaka ya kipalestina wako imara kulinda usalama kuelekea katika eneo la Manger Syuare ambako kuna makanisa mawili lile la Nativity na la mtakatifu Catherine.Huko ndiko mkesha wa Krismas utakapofanyika.

Askofu wa Katoliki wa Mashariki ya Kati Latin Patriarch Fuad Twal ndiye atakayeongoza misa ya mkesha huo.

Atatoa ujumbe wa matumaini ya amani, lakini pia ataelezea masikitiko yake kuhusiana na mauaji ya waumini wa kikristo katika kanisa moja mjini Baghdad.Wakristo nchini Iraq wamekuwa wakishambuliwa mara kwa mara.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Palestina kiasi cha watu elfu 90 wanatarajiwa kushiriki katika mkesha huo wa Krismas.

Mwandishi:Aboubakary Liongo/AFP

Mhariri:Abdul Mtullya