Mkosoaji wa serikali ya Tanzania aachiwa baada ya kutekwa
13 Januari 2025Matangazo
Mume wa mwanaharakati huyo aliishutumu idara ya ujasusi ya Tanzania kwa kuhusika na tukio hilo.
Taarifa ya kutekwa kwa Maria Sarungi mtetezi wa haki za binadamu ambaye anakosoa utawala wa rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ziliripotiwa na shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International jana mchana.
Soma pia:Mwanaharakati wa Tanzania Maria Sarungi asema yuko salama baada ya kutekwa nyara Nairobi
Baada muda mfupi baada ya kusambaa kwa taarifa hizo, Mwanaharakati huyo alichapisha kwenye mtandao wa kijamii wa X akisema kwamba sasa yuko salama na kuahidi kuuzungumzia mkasa huu hii leo.
Mkasa huo umetokea wakati Tanzania na Kenya zikiwa zinashutumiwa kwa kuwateka nyara wakosoaji.