1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkulima wa Burkina Faso ashinda Tuzo mbadala ya Nobel

23 Novemba 2018

Mkulima mmoja kutoka Burkina Faso ambaye ameipa umashuhuri mbinu ya kilimo inayorutubisha ardhi na kuondoa jangwa ni miongoni mwa washindi wa tuzo mbadala ya Nobel iliyotangazwa siku ya jumatatu.

***SPERRFRIST 24.09.2018 um 09.00 Uhr*****  Right Livelihood Award Yacouba Sawadogo
Picha: Right Livelihood Award/Mark Dodd

Yacouba Sawadogo anapokea tuzo hiyo kwa pamoja na watetezi wawili wa haki za binadamu kutoka Saudi Arabia na mkulima mmoja kutoka Australia. Tuzo hiyo yenye thamani ya dola za Marekani 341,800 hutunukiwa watu wanaotafuta suluhisho kwa matatizo ya ulimwengu.

Sawadogo anafahamika kwa kubadili sehemu kubwa ya ardhi isiyo na rutuba kuwa msitu na eneo linalofaa tena kwa kilimo kwa kutumia mbinu iitwayo "Zai”.

Mbinu hiyo inahusisha uchimbaji wa ambapo mashimo madogo ardhini ambayo huruhusu kukusanyika kwa maji na virutubisho vingine vinavyowezesha mimea kukua na kukabili ukame.

Kulingana na wakfu wa Right Livelihood unaosimamia tuzo hiyo mbinu ya ‘Zai' imekuwa ikitumika kurejesha rutuba katika maelfu ya hekari za ardhi kavu na kupunguza baa la njaa nchini Burkina Fasso na Niger tangu Sawadogo alipoanza kuifundisha katika miaka ya 1980 

Sawadogo amesema kuwa anatumai ataitumia tuzo hiyo kwa manufaa ya siku za usoni.

"Matarajio yangu ni kwa watu kujifunza maarifa niliyonayo na kuyasambaza kwa wengine. Hilo linaweza kuwanufaisha vijana” Sawadogo ameliambia shirika la Habari la Reuters kwa njia ya simu akiwa kijijini kwake nchini Burkina Faso.

Burkina Faso inaelekea kuwa nusu jangwa

Picha: Getty Images/AFP/I. Sanogo

Wataalam wamesema Burkina Faso imo kwenye hatari ya kutumbukia kwenye ukanda wa nusu jangwa uliopo kusini mwa jangwa la sahara unaofahamika kama Sahel ambapo mabadiliko ya tabianchi na matumizi ya ardhi yaliyopindukia yanasababisha kuwa vigumu zaidi kwa wakaazi wa maeneo hayo kulima.

"Yacouba Sawadogo aliahidi kuzuia kutokea kwa jangwa na amefanikiwa.” Amesema Ole von Uexkull, mkurugenzi mtendaji wa wakfu wa Right Livelihood unaosimamia tuzo hiyo mbadala ya Nobel.

Uexkull ameongeza kusema kuwa ikiwa wataalamu wa ndani na wale wakimataifa wataamua kujifunza mbinu ya Sawadogo itakuwa rahisi kuyaokoa maeneo mengi yanayokabiliwa na hali ya jangwa na ukosefu wa rutuba jambo litakalosaidia kupunguza kuhama hama kwa watu na kuimarisha amani kwenye ukanda wa Sahel.

Mwaka jana, mvua zisizotabirika ziliwaacha kiasi watu millioni wakiwa hawana chakula na kuhitaji chakula na kuhitaji msaada kote nchini Burkina Faso.

Mbinu yake ilipingwa hapo kabla

Picha: DW

Hapo kabla mkulima huyo alikabiliwa na upinzani mkubwa kutokana na njia hiyo kuwa na isisokubalika miongoni mwa wataalam wa masula ya ardhi na ilizingatiwa kuwa ya kale na iliyoshindwa.

Hivi sasa mbinu ya „zai" ndiyo inatumika kwa sehemu kubwa na mashirika ya kutoa misaada yanayofanya kazi ya kuzuia baa la njaa katika eneo la Sahel.

Sawadogo alihadhithia simulizi yake katika filamu iliyorekodiwa mwaka 2010 iliyopewa jina la "Mtu aliyezuwia jangwa”

Mwandishi: Rashid Chilumba

Mhariri: Iddi Ssessanga

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW