Mkutano kati ya Ujerumani na Urusi
19 Julai 2011Matangazo
Rais wa Urisi Dmitr Medvedev amewasili nchini Ujerumani hapo jana kwa mazungumzo na Kansela Angela Merkel.
Viongozi hao wanakutana katika mji uliopo kaskazini, Hanover, kwa kikao cha pande mbili cha siku mbili. Ni mkutano wa 13 wa kila mwaka wa viongozi wa kisiasa na kibiashara kutoka nchi hizo mbili.
Huenda uhusiano unaokuwa wa kibiashara kati ya Ujerumani na Urusi ndio ukatawala kikao hicho. Ujerumani ni mshirika wa kipekee wa muhimu kibiashara kwa Urusi ,na Urusi ni muuzaji mkubwa wa nje wa nishati kwa Ujerumani.
Mwandishi:Maryam Abdalla/afp, dapd
Mhariri:Kitojo Sekione