1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano kuhusu Mlango-Bahari wa Hormuz kufanyika London

22 Aprili 2026

Wataalam wa kijeshi kutoka nchi zaidi ya 30 watakutana Jumatano mjini London katika mkutano wa siku mbili utakaojadili namna ya kuhakikisha ulinzi katika Mlango-Bahari wa Hormuz mara tu vita vya Iran vitakapomalizika.

Viongozi wa Ulaya wakijadiliana kuhusu kuulinda Mlango-Bahari wa Hormuz
Viongozi wa Ulaya wakijadiliana kuhusu kuulinda Mlango-Bahari wa HormuzPicha: Tom Nicholson/AFP

Mkutano huo utakaoongozwa na Uingereza na Ufaransa, unalenga kuandaa mikakati madhubuti wa kulinda meli za mafuta, kama walivyojadili wiki iliyopita mjini Paris, Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Mazungumzo hayo yatakayofanyika huko Northwood kaskazini mwa jiji la London yatazingatia uwezo wa kijeshi, masuala ya amri na udhibiti, kutegua mabomu ya ardhini na jinsi vikosi vya kijeshi vinavyoweza kupelekwa katika eneo hilo la Mlango-Habari wa Hormuz.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW