Mkutano unaodurusu shughuli za mahakama ya ICC wamalizika Kampala
11 Juni 2010Matangazo
Kongamano la kwanza la kuurekebisha mkataba wa Roma wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu- ICC- ambalo limekuwa likifanyika mjini Kampala kwa wiki mbili sasa, na ambalo linafaa kumalizika leo limegeuka kuwa gumu kwani wajumbe bado wanatafautiana kuhusu jinsi uchunguzi wa makosa ya uchokozi unavofaa kufanyika.
Wakati tukianza matangazo yetu, wajumbe walikuwa bado wanaendelea na majadiliano wakitumai kuafikiana.
Mwandishi wetu Leyla Ndinda kutoka Kampala ametutumia taarifa ifuatayo
Mwandishi, Leyla Ndinda
Mhariri, Othman Miraji