1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Njia za kumaliza vita vya Urusi na Ukraine zajadiliwa Uswisi

16 Juni 2024

Mataifa ya Magharibi na mataifa mengine duniani yatatumia siku ya pili ya mkutano wa kimataifa wa kujadili amani unaofanyika nchini Uswisi, kutafuta uungwaji mkono wa pamoja wa kukosoa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine

Bürgenstock | Uswisi
Mkutano wa amani wa Uswisi unatafuta njia za kumaliza vita vya Urusi na UkrainePicha: Alessandro Della Valle/POOL/AFP/Getty Images

Mkutano huo pia utaangalia athari ya vita kwa maisha ya binaadamu.

Rasimu iliyoonekana na shirika la habari la Reuters, inauelezea uvamizi wa Urusi nchini Ukraine kama vita, jambo ambalo Moscow inaendelea kulikanusha ikisema ni operesheni maalum ya kijeshi. Rasimu hiyo pia imetoa wito wa kuachiwa kwa kinu cha nyuklia cha Ukraine kinachodhibitiwa na Urusi cha Zaporizhzhia pamoja na bandari ya Azov. 

Vita vya Urusi nchini Ukraine vimeendelea kusambaratisha uhusiano wa taifa hilo na nchi za Magharibi ambapo Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema mataifa hayo yanataka kuifanya Urusi kuyanyenyekea.

Mkutano wa kimataifa wa amani Ukraine wafungua Uswisi

Viongozi wa dunia akiwemo makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wamekusanyika katika eneo la  la mapumziko la Bürgenstock ili kutafuta uungwaji mkono wa Kimataifa wa kumaliza vita hivyo. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW