Mkutano wa APEC kuanza leo Korea Kusini
31 Oktoba 2025
Viongozi wa mataifa 21 yaliyopo kwenye Jumuiyaya ushirikiano wa kiuchumi wa nchi za Asia na Pasifiki wanatarajiwa kufungua mkutano wao wa kilele wa kila mwaka Ijumaa hii huko Korea Kusini kujadili jinsi ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kukabiliana na changamoto zinazowakabili.
Mkutano huo wa siku mbili unafanyika katika mji wa Gyeongju ikiwa ni siku moja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump aliyekuwa barani Asia kukutana na mwenzake wa China Xi Jinping na kukubaliana kuchukua hatua za kupunguza vita vyao vya kibiashara.
Jumuiya ya APEC ilianzishwa mwaka 1989wakati wa ongezeko la utandawazi, na inawakilisha zaidi ya nusu ya biashara ya kimataifa. Jukwaa hilo linatetea mfumo wa biashara huru na waz. APEC inapewa sifa ya kuzileta pamoja nchi zilizokuwa na ushindani ili kushirikiana katika mipango ya pamoja.