1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mkutano wa ASEAN kujadili usalama unafanyika leo Indonesia

Angela Mdungu
14 Julai 2023

Wanadiplomasia wa ngazi ya juu kutoka Marekani, China na Urusi sambamba na mawaziri wa masuala ya kigeni wa Mataifa ya kusini mashariki mwa Asia hivi leo wanahudhuria mkutano wa kiusalama huko Indonesia.

Indonesien Südostasien Wang Yi und Antony Blinken
Picha: Dita Alangkara/AP Photo/picture alliance

Wanadiplomasia wa ngazi ya juu kutoka Marekani, China na Urusi sambamba na mawaziri wa masuala ya kigeni wa Mataifa ya kusini mashariki mwa Asia hivi leo wanahudhuria mkutano wa kiusalama huko Indonesia. Kati ya mambo yanayopewa uzito kwenye mkutano huo ni pamoja na mzozo wa bahari ya kusini ya China, vita vya Ukraine pamoja na makombora ya Korea kaskazini.

Mkutano huo wa jumuiya ya mataifa ya kusini mashariki mwa Asia ASEAN, yenye nchi 27 wanachama unatoa pia nafasi kwa mataifa yenye nguvu kujadili juu ya masuala mbali mbali wakati wa mjadala wao wa faragha.

Soma zaidi:Indonesia yaridhishwa na ushirikiano wa China kwa amani ya Myanmar

Wakati mivutano ya China na Marekani ikishika kasi kuhusu kisiwa kinachojitawala cha Taiwan, pamoja na  uhusiano wa karibu kati ya China na Urusi, bila kusahau mzozo juu ya ushawishi kusini mwa Pasifiki, Indonesia ambayo ndiyo mwenyeji wa mkutano huo ilishatahadharisha kuwa Jumuiya ya ASEAN haiwezi kutumiwa kama wakala wa mizozo

Waziri wa mambo ya nje wa Indonesia Retno MarsudiPicha: Agung Pambudhy/detikcom

Awali alipokuwa akifungua mkutano wa mataifa 18 ya  mashariki mwa Asia, waziri wa masuala ya kigeni wa Indonesia Retno Marsudi aliwaambia mawaziri wenzake kuwa, eneo la Indo-Pasifiki halipaswi kugeuka kuwa uwanja mwingine wa mapambano.

Walaani machafuko ya Myanmar

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa jumuiya hiyo wametahadharisha pia kwa mara nyingine na kulaani mashambulizi ya anga na mizinga pamoja na vurugu nchini Myanmar. Hata hivyo wamekuwa na mawazo tofauti juu ya kuumaliza mzozo nchini humo.

Mkutano huo unahudhuriwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken, mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa China Wang Yina waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov wakiwa ni chombo kilichoundwa kujadili masuala ya kiusalama yanayohusisha pia nchi za Japan, Korea kusini na Australia.

Mkutano huu ni kwanza kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani na Urusi tangu walipokutana kwa muda mfupi mwezi Machi nchini India. Hata hivyo, hakutarajiwi kuwa na mazungumzo yoyote kati ya Blinken na Lavrov wakati ambapo Urusi inalaumiwa kwa uvamizi wake nchini Ukraine.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW