1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Baba mtakatifu na waislamu

26 Septemba 2006

Mada 2 zilitia fira leo katika safu za wahariri wa magezti ya Ujerumani: mkutano wa baba mtakatifu Benedikt na waakilishi wa kiislamu na bima ya afya inayozusha mvutano katika serikali ya muungano ya Ujerumani.

Baba mtakatifu akikutana na waakilishi wa kiislamu
Baba mtakatifu akikutana na waakilishi wa kiislamuPicha: AP

Gazeti la Dresdner Neusten Nachrichten laandika:

„Baba mtakatifu ameelezea mara 4 masikitiko yake

lakini kamwe, hakufika umbali wa kujidhalilisha.Kinyume chake:Matarajio ya Benedikt ya kufufua upya maelewano taabu sana baina ya wakristu na waislamu, yalitimilia kutokana na mkutano aliofanya na wajumbe wa kiislamu katika qasri la Castel Gandolfo.Pande hizo mbili, zilizungumza na hasa juu ya matatizo yaliopo.Mabingwa wa maswali ya Vatikani hawakumbuki baba mtakatifu yupi alierejea kuchambua maneno yake aliosema mara kwa mara.“

Gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung laandika:

„Kuamini kwamba Baba mtakatifu hajakusudia kwa dhati aliyoyasema Regensburg,si sawa. Baba mtakatifu alimnukulu mfalme wa enzi za Byzantin, aliekabiliana na wimbi la kujitanua kwa uislamu ambako haraka kungeuzika ukristu katika mashariki ya kati na ya mbali.

Leo hii, ukristu wa ulimwengu wa magharibi unajikuta ukikabiliwa na hatari sawa na yaenzi zile. Wapinzani wake hawatumi zaidi silaha, bali kutoamini mungu na kutapia mali…“ Ni maoni ya FAZ.

Gazeti la KIELER NACHRICHTEN linaupongeza pia mkutano aliouitisha Baba mtakatifu na waakilishi wa dini ya kiislamu huko Vatikan hapo jana:

Laandika:

„Baba mtakatifu Benedikt ameegemea zaidi vikundi vya wastani vya ulimwengu wa kiislamu na hapo amefanyavyema.Ghadhabu zilizoibuka tena huko Mashariki ya Kati, zinatoa sura ya uhasama na hii yaendelea kupalilia uhasama.Hicho ndicho hasa wachochezi miongoni mwa waislamu watakavyo.Haifai kwahivyo, kujinasisha katika mtego wao.

Kinachohitajika, ni mchanganyiko wa hatua za wastani za kuambiana bila kufumbia macho ghadhabu kali zilizoibuka katika ulimwengu wa kiislamu.Pia mtu asiyadharau matatizo tulionayo katika kuwajumuisha waislamu na jamii zetu.“

Lituhetimishia mada hii, gazeti la LANDHUTER ZEITUNG/STRAUBINGER TAGBLAT linapongeza pia juhudi alioichukua baba mtakatifu kukutana na waakilishi wa kiislamu:

Laandika,

„Dai la wale wenye msimamo mkali kudai baba mtakatifu atake radhi kwa alioyasema,hakuliitikia.Na hakuwa na sababu ya kutaka radhi.Hata matamshi yake ya jana, hayawezi kutafsiriwa ni kuupiga magoti uislamu.Baba mtakatifu Benedikt XVI, amependekeza mazungumzo ya kweli yatakayoweza kuchangia kupunguza tena kwa pamoja mvutanouliopo.“

Likigeukia ya mageuzi ya bima ya afya humu nchini, gazeti la BERLINER MORGENPOST,laandika:

“Seriali ya mungano ya Ujerumani yaonesha ukubwa wake upo katika idadi yake ya wabunge tu.Katika siasa za kawaida, vyama vya SPD na CDU/CSU vimetumbukia katika mivutano midogo-midogo ya kichama na vimeshaagana na ahadi vilivyotoa kutumia wingi wao Bungeni kupitisha mageuzi.Wananchi wanaihisi hali hiyo na wamevunjwa moyo.

Serikali ya vyama vikuu yabainika imeamua kutopitisha mambo mengi.Yafaa kwa upande mwengine, kupendekleza kwa wananchi kwamba, hadi vyama hivyo vitakapoafikiana wasiwatie maanani wasemayo wanasiasa hao.”

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW