1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Baerlin wa sheria za kuyadhibiti masoko ya fedha Berlin

20 Mei 2010

Bibi Angela Merkel akosolewa kujiamulia peke ?

Chancellor Angela MerkelPicha: AP

Ujerumani leo imeitisha kuwepo na sheria kali za kuyadhibiti masoko ya fedha .Ufaransa ikachukua msimamo mkali juu matumizi yake m akubwa na Ugiriki ilikabiliwa na maandamano zaidi mitaani huku eneo la nchi za sarafu ya Euro likipigana kupambana na msukosuko wa madeni na tofauti zilizochomoza kati yao.Ramadhan Ali na kikao kilichofanyika leo mjini Berlin kukabiliana na msukosuko wa fedha:

Masoko ya hisa yakiyumba-yumba kutokana na hatua isiotazamiwa iliochukua Ujerumani kukaba biashara ya ulanguzi kwenye masoko ya fedha, Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani, alishinikiza leo haja ya kutozwa kodi maalumu masoko ya fedha ili kuweza kudhibiti ubadhirifu unaolaumiwa kuchangia msukosuko wa fedha duniani.

Kanzela Merkel , aliuambia leo mkutano maalumu mjini Berlin leo uliozingatia sheria za kupambana na walanguz :

" Naamini kuwa, yawezekana hata katika ulimwengu huu wa utandawazi tukatunga mfumo ambamo nguvu za masoko ndizo zinazosukuma mbele uchumi ,lakini wakati huo huo, zimedhibitiwa na muongozo wa kisiasa kwa njia ambayo, hazichafui sera za kisiasa bali zinaziendeleza mbele."

Kanzela Merkel akasema zaidi,

"Tumetamka kwamba tutapiga kampeni ya kutozwa kodi masoko ya fedha na tutaipigia kampeni kodi hiyo wakati wa mkutano wetu wa nchi 20-tajiri kabisa duniani nchini Kanada."

Kuhusu sarafu ya Euro kutiwa msukosuko, kunakotokana na madeni ya baadhi ya nchi zinazotumia sarafu ya Euro,Kanzela Merkel, alisema ,

" Kunahitajika sheria kali zaidi kuliko ilivyo kwa zile serikali zinazojiamulia binafsi juu ya sarafu zao ."

Kanzuela Merkel, akasema pia kuwa panahitajika kuimarisha zaidi yale mapatano ya kuimarisha sarafu na ukuaji uchumi.Alitoa dai hilo kabla ya mkutano wa mawaziri wa fedha wa Umoja wa Ulaya, uliopangwa hapo kesho Ijumaa mjini Brussels,Ubelgiji.

Waziri wa fedha wa Ujerumani Bw.Wolfgang Schäuble, waziri wa fedha wa Ufaransa bibi Christine Lagarde, ambae ni miongoni mwa wale waliomkosdoa Kanzela Merkel, kwa kujiamulia mambo pekee pamoja na Kamishna wa maswali ya uchumi wa Umoja wa Ulaya, Michel Barnier,walihudhuria mkutano wa leo mjini Berlin.

Kanzela Merkel alisababisha mtafaruku hapo jana pale serikali yake mjini Berlin ilipopiga marufuku uuzaji wa dhamana au hisa kwa wafanyabiashara masokoni ambao hawana dhamana ya fedha wanazotumia au wamezikopa kwa biashara yao ya ulanguzi.

Lakini, ikiwa hatua hiyo ya kuwapiga hao marufuku ilikusudiwa kuzuwia kuanguka zaidi thamani ya Euro,ilishindwa kutimiza shabaha yake.Kwani , hatua hiyo ilitikisa masoko ya fedha ulimwenguni na kuzidi kuiangusha thamani ya Euro na kufikia kipimo cha chini kabisa ambacho hakikufikiwa tangu miaka 4. Hii imechochewa pia na hofu za wawekezaji kuwa , mzozo wa madeni wa Ulaya, unaoenea utautosa uchumi wa ulaya na pengine wa dunia kurudi kuzorota kama ilivyokuwa hapo kabla.

Hapo awali, waziri wa fedha wa Ufaransa,Christine Lagarde, aliambia radio RTL kuwa,Ufaransa, haitafuata nyayo za Ujerumani na haikubaliani na onyo la Kanzela Merekel , kuwa sarafu ya Euro, kweli iko hatarini.

Msukosuo uliopo ulaya, unachochewa na madeni na nakisi katika hazina za serikali ambazo zimepindukia kipimo cha juu kilichowekwa na kanuni za Umoja wa Ulaya na kuwa serikali zimongeza matumizi kupita kiasi ili kuwezesha uchumi wao kujiokoa na hali ya kuzorota .

Sasa zinatakiwa zilipe madeni huku riba ikiwa juu sana .Na hali hii, inapelekea hazina za serikali kuzidi kudhofika na kupelekea ile hali iliojikuta Ugiriki ya kuomba Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha Ulimwenguni, kuitia jeki kwa kima cha Euro bilioni 110 mapema mwezi huu.

Mwandishi: Ramadhan Ali/ AFPE

Mhariri:Abdul-Rahman

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW