1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa waendelea New York

24 Septemba 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ameuhutubia mkutano huo akizungumzia vinavyoendelea nchini mwake, ambapo ameonya kwamba Urusi inapanga kuvieneza vita kote barani Ulaya na kuutaka Umoja wa Mataifa kuingilia kati.

 2025 | Volodymyr Zelenskyy
Rias wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akihutubia mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa MataifaPicha: Selcuk Acar/Anadolu/picture alliance

Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaendelea hii leo ambapo viongozi mbalimbali wameendelea kutoa hotuba zao.

Jioni hii, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ameuhutubia mkutano huo mjini New York, akizungumzia vinavyoendelea nchini mwake, ambapo ameonya kwamba Urusi inapanga kuvieneza vita kote barani Ulaya na kuutaka Umoja wa Mataifa kuingilia kati.

Rais Masoud Pezeshkian wa Iran naye amehutubia mkutano huo ambapo amevigusia vita huko Mashariki ya Kati huku akimtaja Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kama muhalifu wa kivita na kwamba Umoja wa Mataifa unapaswa kuchukulia hatua dhidi ya Israel kwa vitendo vyake huko Gaza.

Rais wa Syria Ahmad Al- Sharaa ambaye ni kwa mara yake kuhudhuria mkutano huo baada ya kumuondoa madarakani Bashar al Assad ni miongoni mwa wanaohutubia mkutano huo hii leo.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW