Mkutano wa Berlin kuhusu Libya mwakani
25 Novemba 2019Matangazo
Katika ziara yake nchini Libya mwishoni mwa mwezi Oktoba, Waziri wa Mambo ya kigeni wa Ujerumani, Heiko Maas alielezea matumaini yake kwamba mkutano huo wa kilele utafanyika mwaka huu.
Libya ilitumbukia katika machafuko tangu kuondolewa madarakani kiongozi wake wa muda mrefu Moamar Gaddafi mwaka 2011na tangu wakati huo serikali mbili nchini humo zinawania madaraka huku makundi kadhaa ya wapiganaji yakipambana kuchukua udhibiti wa mji mkuu, Tripoli.
Tangu mwezi Septemba, Ujerumani imekuwa ikijaribu kuwa mpatanishi katika mzozo wa Libya, kwa matumaini ya kuzuia kuibuka vita kama vya Syria.