1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MKUTANO WA CLUB YA PARIS KUSIMAMISHA MALIPO YA MADENI KWA NCHI ZILIZOPATWA NA MAFURIKO ASIA:

12 Januari 2005

Serikali zinazodai fedha zanachama wa ‘PARIS CLUB’ zaelekea zikaridhia katika kikao chao cha leo kusimamisha malipo ya madeni yao kwa nchi zilizokumbwa na msiba wa mafuriko ya Tsunami nchini Indonesia,Sri Lanka na hata visiwa vya Seyschelles.

Jana tayari mkutano wa wafadhili mjini Geneva uliofanyika chini ya paaa la UM na wapili baada ya ule wa Jakarta wiki iliopita,ulimalizika kwa mafanikio.Wafadhili huko waliahidi msaada wa kwanza wa dharura wa kima cha dala milioni 717 kati ya kima kilichoombwa na Katibu mkuu wa UM Kofi Annan.

Wanachama wengi wa hiyo inayoitwa ‘PARIS CLUB’ inayowakusanya pamoja nchi 19 zinazodai fedha kwa mikopo yao walikwishatoa mwito wa kusimamisha malipo ya madeni yao kwa sasa kwa nchi zilizokumbwa na msiba wa Tsunami za Kusini mashariki mwa Asia ambazo zimeomba kupunguziwa mzigo huo.

Indioa na Thailand zimebainisha lakini kuwa katika kikao cha leo cha Paris Club mjini Paris, hazitaomba kusimamishiwa kulipa madeni yao kwavile masharti ya mikopo yaweza yakafanya kwa shida kwao kupata mikopo mipya au hata kupewa mikopo kwa masharti magumu katika soko la fedha ulimwenguni.

Shirika linaloratibu mikopo ‘FITCVH’ katika taarifa lililotoa limesema ‘kuahirisha kulipa madeni ya nchi za nje kunaweza baadae kukatatanisha malipo ya madeni.’

Indonesia lakini,itakumbana na shida katika kupunguziwa mzigo wa madeni,kwani deni lake inayodaiwa na nchi za nje linafikia dala bilioni 132 na inatafuta mkopo wa kiasi cha dala milioni 3 mwaka huu kulihudumia tu deni hilo.

jana waziri wa nje wa Ufaransa,Michel Barnier alisema kuwa Ufaransa itayari kutoa nafuu za madeni kwa hadi kima cha Euro milioni 130 ikiwa Indonesia itaahidi kutumia fedha hizo kwa kazi ya kujenga upya maeneo ya maafa.

Deni la Sri Lanka inayodaiwa na nchi za nje ni kiasi cha dala bilioni 7.7 na deni inayodaiwa Seyschelles laweza pia kujadiliwa katika mkutano huu wa Paris Club.

Club ya Paris imearifu kwamba kusimamisha malipo ya madeni kwa muda ni hatua ya kwanza tu katika njia ndefu ya kuzisaidia nchi zilizopatwa na maafa ya zilzala na mafuriko ya Desemba 26 mwaka jana na yaliohilikisha kiasi cha watu 157,000.

Hatua za kupunguziwa madeni au kuyarekebishwa chini ya mfumo mpya zitapaswa kusubiri tathmini ndefu ya msiba huu mkubwa ulioikumba Asia kutoka Banki Kuu ya Dunia na Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF).

Kwa jicho la mashirika yasio ya kiserikali-NGOs,kutunga mfumo mpya wa kulipa madeni au kusimamisha tu kulipwa madeni hakutoshi kabisa katika kuzisaidia nchi zilizokumbwa na maafa haya.

Kwa jicho hilo maandamano yamepanbgwa kufanyika leo nje ya wizara ya fedha ya Ufaransa mjini Paris ambako kikao hiki cha PARIS CLUB kinafanyika leo ili kudai madeni ya nchi zilizoathiriwa na mafuriko ya Tsunami yafutwe kabisa.yanadai halkadhalika UM uitishe mkutano wa kimataifa ukiwa na ajenda hiyo.

Katika kikao cha jana mjini Geneva, uswisi ,wafadhili walijitolea mchango wa dharura wa dala milioni 717.Na mjumbe wa UM anaeongoza misaada kwa nchi zilizokumbwa na mafa haya Jan Egeland alisema,

"Ilikua isahara ya kutia moyo mno kutoka mkutano huu:Ulimwengu una azma ya kuonesha huu ni mchango mkubwa kabisa uliowahi kufanyika na sio kwa jicho la ukarimu,haraka na kuongoza mambo barabara bali pia kwa jicho la kuendesha barabara kabisa uejnzi mpya ambao kwa sehemu umeshaanza."-alisema Egeland.

Kwa jicho hilo la kzijenga upya nchi hizo,Banki kuu ya dunia na Banki ya Asia ya ujenzi mpya zimeahidi huko Geneva jana zitachangia mno.

Waziri wa misaada ya maendeleo wa Ujerumani akihudhuria pia mkutano huo huko Geneva, Bibi Heidemarie Wiezorek-Zeul alionya kwamba fedha za kuzijenga upya nchi zilizoathiriwa na mafuriko ya Tsunami ziszoke katika mfuko wa fedha za misaada zilizowekwa kando kwa nchi nyengine zilizopatwa na maafa.

Alisema,"Nnaweza kuwaambia wazi wazi michango ilioahidiwa hapa ni fedha nyengine kabisa.Msaada kwa nchi za Kusini-mashariki mwa Asia ni mwengine kabisa na ni zaidi."

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW