1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Darfour mjini Addis Ababa

16 Novemba 2006

AddisAbaba

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa kofi Annan yuko ziarani mjini Addis Ababa Ethiopia kushiriki katika mazungumzo kuhusu jimbo la Sudan- Darfour.Mazungumzo hayo ya Darfour yameitishwa na mwenyewe katibu mkuu wa umoja wa mataifa kwa ushirikiano pamoja na mwenyekiti wa kamisheni ya Umoja wa Afrika Alpha Oumar Konare.Wawakilishi wa nchi tano za baraza la usalama la umoja wa mataifa wanahudhuria mkutano huo pamoja na wenzao wa kutoka jumuia ya nchi za kiarabu,Misri,Umoja wa ulaya,,Gabon na Congo Brazaville - mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika.Lengo la mkutano huo ni kutathmini hali katika jimbo la Darfour na kuchunguza namna ya kuupa msukumo utaratibu wa amani.