1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa G20 kutawaliwa na siasa za ndani

27 Juni 2019

Mkutano wa viongozi kutoka mataifa 20 yaliyo na utajiri mkubwa duniani yaani G20 unatabiriwa kwamba utazingatia zaidi siasa za mataifa hayo kuliko maswala ya kidiplomasia ya kimataifa.

G20 Osaka Japan
Picha: picture-alliance/dpa/K. Ota

Kwa viongozi wa Umoja wa Ulaya watalenga kuwahimiza wakuu wa mataifa G20 kusaidia katika kubadilisha sheria za Shirika la Biashara Ulimwenguni, WTO, kwa lengo la kuhifadhi sheria za kibiashara ambazo ziko katika tishio kutokana na kuendelea kwa vita vya kibiashara baina ya Marekani na China. Mkuatano huo unatazamiwa kutawalwa na mada ya mabadiliko ya tabia nchi pamoja na usawa na biashara huru kimataifa.

Kiongozi wa Umoja wa Ulaya, Donald Tusk, na mkuu wa kamishina kuu ya umoja huo, Jean-Claude Juncker walieleza katika barua yao kwamba watasukuma mkutano huo kuendelea kujadili marekebisho ya sheria za biashara za WTO kama ilivyokubalika katika mkutano wa mwaka jana.

"Tutaendesha huu mchakato kwa kuhakikisha marekebisho ya kisawa sawa yanazingatia hoja tatu muhimu za shirika la biashara duniani moja ikiwa ni kusimamia, kujadili na kusuluhisha mizozo," waliandika wakuu hao wa Umoja wa Ulaya.

Rais Donald Trump na waziri mkuu wa Australia Scott Morrison katika chakula cha jioni kabla ya mkutano wa G20Picha: Reuters/K. Lamarque

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Peter Apps alisema kwamba Rais wa Marekani, Donald Trump hoja zake muhimu zitakuwa ni ufanisi wa biashara na kufanikisha uhusiano na mataifa rafiki kwa ajili ya kampeni zake za kuchaguliwa tena katika uchaguzi mkuu wa 2020. Kuna uwezekano kwamba mazingatio yake makubwa yapo katika mjadala wa wanaotaka kuwania urais katika chama cha Demorat kuliko jambo jengine lolote katika mkutano huo wa G20.

Zaidi inaelezwa kwamba Trump na wakaribu wake wanafuatilia kwa ukaribu sana mzozo wake na Iran, mzozo ambao unaonyesha kabisa namna kila upande umediriki kwa hasara yoyote ile kuonyesha ubabe bila kujali athari za kuharibika kabisa kwa uhusiano wa mataifa hayo.

China haitaki Hongkong kujadiliwa

Kuhusu China na Marekani, rais wa China Xi Jinping atasisitiza kuepukwa kwa mijadala kuhusu masuala ya ndani ya nchi yake hasa kuhusiana na mgogoro wa Hongkong juu ya mswada wa sheria wa wahalifu kupelekwa katika mahakama za China. China ilisema haitaruhusu maandamno ya Hongkong kujadiliwa katika mkutano huo wa G20 japo kunatarajiwa kuwa na waandamanaji nje ya majengo kutakamofanyika mkutano huo.

Rais wa Uturuki Recep Tayyib na mkewe wakiwasili Jaban Picha: picture-alliance/dpa/M. Cetinmuhurdar

"Mataifa mengi yana wasiwasi juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini China hasa kuwekwa katika vizuizi vya mateso kwa waisilamu zaidi ya milioni moja wa jamii ya Uighur, swala hili kuna uwezekano rais Turmp akaliibua kwa rais XI," alisema mchambuzi Peter Apps.

Viongozi wengine wa mataifa ya Magharibi nao watahisi kuendelea kupotzea nguvu zao kama vile waziri mkuu wa Uingereza Theresa May baada ya kutangaza kwamba atajiuzulu naye Kansela wa Ujermani, Angela Merkel alijizulu kama kiongozi wa chama cha Kikristo cha Democrats na anakabiliwa na maswali kuhusiana na afya yake. Naye rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau wanakabiliwa na hali nghumu nchini mwao na kuna uwezekano wa kushindwa katika uchaguzi ujao huku rais wa Uturuki, Tayyip Edrgan uimara wake kuonekana kuanza kupungua kwa chama chake cha AK kushindwa katika marudilio ya uchaguzi huko Instanbul.

(RTRE)

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW