1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa G20 wahitimishwa Brazil

20 Novemba 2024

Siku ya mwisho ya mkutano wa viongozi wa nchi zenye uchumi mkubwa zaidi duniani G20 iligubikwa na mjadala kuhusu vita vya Ukraine huku pande zote zikitupiana lawama kuuchochea mzozo huo.

Mkutano wa G20 nchini Brazil
Mkutano wa G20 nchini BrazilPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Hatua ya Marekani kuiruhusu Ukraine kutumia makombora yake ya masafa marefu kushambulia miundombinu ya kijeshi ndani ya Urusi imeibua wasiwasi  kwa washirika wa Ukraine barani Ulaya, hasa baada ya Urusi kutishia kutumia silaha zake za nyuklia.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemtaka mwenzake wa China Xi Jinping kutumia ushawishi wake kwa kiongozi wa Urusi Vladimir Putin. China na Brazil wamesema wanaunga mkono njia ya mazungumzo ili kuumaliza mzozo huo.

Mkutano huo wa siku mbili wa  G20 , ulihitimishwa na ombi la Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva kwa viongozi wenye nguvu zaidi duniani kuchukua hatua za kuwezesha kufikiwa makubaliano kwenye mazungumzo yaliyokwama katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa wa hali ya hewa wa COP29 huko Azerbaijan.

     

     

  

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW