Mkutano wa hali ya hewa mjini Bonn
29 Machi 2009Bonn:
Mkutano kuhusu makubaliano ya kimataifa ya kuhifadhi hali ya hewa umefunguliwa hii leo mjini Bonn nchini Ujerumani.Mkutano huo ni maandalizi ya mkutano wa kilele wa Copenhagen,december mwaka huu utakaopitisha makubaliano yatakayochukua nafasi ya itifaki ya Kyoto ambayo muda wake unamalizika mwaka 2012.Kwa jumla mkutano huo wa Bonn umelengwa kusaka njia maadhubuti za kupunguza moshi wa viwandani unaochafua mazingira na kuzisaidia nchi zinazoinukia katika juhudi zao za kukabiliana na kishindo cha mabadiliko ya hali ya hewa.Wajumbe elfu mbili kutoka mataifa zaidi ya 180 wanahudhuria mkutano huo wa siku kumi mjini Bonn.Wakati huo huo rais Barack Obama wa Marekani amewaalika viongozi wa mataifa 16 muhimu zaidi kiuchumi washiriki katika mkutano wa kilele wa hali ya hewa,utakaofanyika mjini Washington mwishoni mwa mwezi ujao wa April.