Mkutano wa IAEA waanza leo
7 Septemba 2009Mkutano huo utajadili madai kwamba Iran ilifanya utafiti ulio na azma ya kutengeza mabomu ya nuklia vilevile madai kwamba Syria ilikuwa na harakati za kutengeza kinu cha nuklia kabla ya kuvamiwa na Israel mwaka 2007.
Shirika hilo lililo na nchi 35 wanachama linahusika na usimamizi wa kusambaa kwa silaha na teknolojia ya nuklia.
Kile kilicho muhimu kinalindwa sana. Kwa idara hii ya uchunguzi, wafanyakazi wanachunguza maeneo ya kinuklia kutoka duniani kote ili kuweza kuweka pamoja uchunguzi wao. Iwapo mtu anataka kuingia katika ukumbi huo kwanza lazima atoe taarifa na kisha atafunguliwa milango maalum ya ukumbi huo. Wachunguzi hapa wanawajibika tu kufanyakazi zao ngumu za siri na sio kuzungumza. Mwalimu wao Jean-Maurice Crete amekuwa kwa miaka kadha akifanyakazi kama mtaalamu wa fizikia ya kinuklia katika nyambizi iliyo na silaha za kinuklia ya jeshi la Ufaransa. Anafahamu mengi kuhusu vinu vya kinuklia, lakini hata silaha za kinuklia. Na anafahamu kile ambacho wachunguzi wanatarajia, wakati akiwa peke yake popote pale katika bara la Asia ama Amerika ya kusini chombo chake kinaweza kuleta kutoka katika kituo cha kinuklia na kuwaeleza wahandisi wadadisi kilichomo katika kamera zinazoangalia vinu hivyo.
Karibu wachunguzi 300 wanaangalia duniani kote kiasi cha maeneo 1,100. Malalamiko mengi ni kuhusu tatizo la wataalamu vijana, vijana ambao wanautaalamu wa fizikia ya kinuklia ni wachache, na katika vituo vya kinuklia wanapata fedha zaidi. Katika shirika la IAEA wanakuja tu wale ambao wana nia halisi, anasema Jean-Maurice Crete. Katika idara yake kila mwaka anapata fedha nyingi, kama nusu ya gharama ya ndege ya kivita. Ni kiasi gani kinatumika kwa ajili ya amani ya dunia? Ukosefu huu wa fedha, haukumshitua pia mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, ambayo aliipata mkuu wa shirika hilo 2005. Na huo ndio ulikuwa ushindi mkubwa wa mkurugenzi mkuu wa IAEA Mohammed el Baradei, na kusababisha kupata zawadi, ambapo alisaidia kupunguza nguvu za madai ya rais George W. Bush kuwa Iraq inamiliki silaha za maangamizi.
Mwanasheria huyo kutoka Misr anaondoka katika wadhifa wa mkurugenzi mkuu wa shirika hilo mwezi Novemba mwaka huu.
Kwa kuaga kwa mara nyingine tena ameonya kutolifanya shirika hilo dhaifu zaidi. IAEA inahitaji haraka kiasi cha Euro milioni 80 ili kufanya ukarabati muhimu , na pia kuwapata wafanyakazi wapya kwa ajili ya kazi ngumu ya shirika hilo. Baradei ameeleza uzoefu wake kwa msisitizo mkubwa.
´´Uwezo wetu wa kutekeleza mfumo wa tathmini ya kinuklia na kugundua uwezekano wa udanganyifu wa mada za kinuklia na shughuli za kinuklia ambazo hazikuwekwa wazi, tayari uko mashakani. Kwa sababu kwa mfano maabara zetu za uchunguzi ni za kizamani na tunakosa uwezo wa kupata picha rasmi za satalite´´.
Bila ya kupata fedha za nyongeza hali hii itakuwa mbaya zaidi. Nafasi ya kurejewa kwa maafa kama ya Chernoble itakuwa kubwa zaidi, iwapo upungufu mkubwa wa wafanyakazi katika mpango wa usalama wa kinuklia hautaangaliwa.
Mwandishi: Eberhard Nembach/ZR/ Sekione Kitojo.
Mhariri :Aboubakary Liongo.