Mkutano wa WEF wafunguliwa rasmi huko Davos,Uswisi
21 Januari 2025Matangazo
Mkutano huo unafanyika siku moja baada ya Donald Trump kuingia madarakani nchini Marekani. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anataka kulitumia jukwaa hilo la kutafuta uungwaji mkono wa nchi yake.
Rais wa Israel Isaack Herzog pia anatarajiwa kuzungumza kwenye jukwaa hili kufuatia kuachiliwa kwa mateka wa nchi hiyo na makubaliano ya kusitisha vita Ukanda wa Gaza.
Kansela Olaf Scholz na mwanasiasa anayegombea ukansela kutoka chama cha kihafidhina nchini Ujerumani cha CDU Fredrich Merz pia watazungumza.
Rais mpya wa Marekani Donald Trump pia anatarajiwa kulihutubia jukwaa hilo siku ya Alhamisi.