1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa jumuiya ya SADC waendelea kwa siku ya pili leo Windhoek

17 Agosti 2010

Ajenda kuu ya kikao hicho ni mbinu za kuuimarisha ushirikiano wa kiuchumi katika kanda hiyo pamoja na masuala ya kisiasa nchini Zimbabwe na Madagscar

Kikao cha kilele cha marais wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Mataifa ya Kusini mwa Afrika,SADC kimeingia siku yake ya pili na kuendelea kwa vikao vya faragha. Kikao hicho kinawaleta pamoja marais 15 wa mataifa wanachama wanaokutana katika mji mkuu wa Namibia, Windhoek.

Ajenda kuu ya kikao hicho ni mbinu za kuuimarisha ushirikiano wa kiuchumi katika kanda hiyo pamoja na masuala ya kisiasa hususan ya Zimbabwe na Madagscar. Ifahimike kuwa kikao hicho kinafanyika ikiwa Jumuiya hiyo imetimiza miaka 30 tangu kuasisiwa. Jumuiya ya SADC inakabiliwa na changamoto nyingi ila imefanikiwa katika baadhi ya masuala.

Muda mfupi uliopita Mohammed Abdulrahman amezungumza na Hashim Mbita Brigadia Jenerali mstaafu wa Tanzania,aliyekuwa pia katibu mkuu wa kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Bara la Afrika kuhusu suala hilo.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi