1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kila mwaka wa chama cha Labour wafunguliwa

Sylvia Mwehozi
22 Septemba 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer ameahidi kulinda huduma za umma na kufutilia mbali hatua za kubana matumizi wakati mkutano wa kila mwaka wa chama cha Labour ukifunguliwa leo.

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer Picha: Simon Dawson/Avalon/Photoshot/picture alliance

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer ameahidi kulinda huduma za umma na kufutilia mbali hatua za kubana matumizi wakati mkutano wa kila mwaka wa chama cha Labour ukifunguliwa leo. Mkutano huo ni wa kwanza katika kipindi cha miaka 15 kufanyika wakati chama hicho kikiwa madarakani.

Mkutano huo wa siku nne wa Liverpool, kaskazini-magharibi mwa Uingereza, unafanyika miezi mitatu baada ya Labour kupata ushindi katika uchaguzi mkuu dhidi ya chama cha Conservatives. Akizungumza na gazeti la Observer la Jumapili, Waziri Mkuu Starmer amesema orodha ya mambo ambayo wameyatekeleza ndani ya wiki 11, yanaonyesha kuwa wamefanya vyema kuliko serikali iliyopita pengine katika miaka 11 iliyopita.

Soma: Starmer aanza 'ujenzi mpya' alioahidi

Kiongozi huyo anayekabiliwa na shinikizo kutoka kila upande, atapaswa kupima uwiano kati ya kusherehekea ushindi wa Labour uliosubiriwa kwa muda mrefu, kutetea rekodi yake na kutoondoa wazo la maamuzi magumu.