kuwepo mfumo wa kuwafidia waliotumika kama watumwa Ghana
17 Novemba 2023Mkutano huo mjini Accra unaongeza mkazo kwenye miito inayoongezeka ya fidia baada ya Waafrika wapatao milioni 12 kuchukuliwa kwa nguvu na kupelekwa Mataifa ya Ulaya kutumikishwa kama watumwa kati ya karne ya 16 hadi 19
Karne nyingi baada ya kumalizika kwa biashara ya utumwa, watu wenye asili ya Kiafrika ulimwenguni, wameendelea kuwa waathiriwa wa ubaguzi wa rangi wa kimfumo pamoja na kukumbwa na mashambulizi ya ubaguzi.
Ziara ya Scholz Afrika na shauku ya kuimarisha uhusiano wa kiuchumi
Hayo ni kulingana na ripoti ya hivi karibuni ya kongamano maalum la Umoja wa Mataifa ambalo liliunga mkono fidia kama kile walichokiita "jiwe la msingi la haki katika karne ya 21."
Amr Aljowailey, balozi na pia mshauri wa naibu mwenyekiti wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Afrika aliyeyasoma maazimio ya mkutano huo amesema fidia inategemea kile alichokiita msingi wa haki za kimaadili na kisheria na utu wa watu.