Mkutano wa kilele wa AU waendelea nchini Ethiopia
15 Februari 2026
Matangazo
Youssouf ametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa kile alichokiita "maangamizi ya watu wa Palestina, kauli iliyomfanya waziri mkuu wa Palestina Mohammad Mustafa, kuishukuru Afrika kwa mshikamano wake.
Youssouf amesema hayo wakati wa mkutano wa 39 wa Umoja huo wa Afrika uliofunguliwa jana mjini Addis Ababa nchini Ethiopia utakaodumu kwa siku mbili.
Mkutano huo wenye kauli mbiu ''maji na usafi wa mazingira'', utajadili mustakabali wa bara hilo lenye idadi ya watu bilioni 1.4.
Mazungumzo yatajumuisha hatua za bara hilo za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na majanga ya kibinadamu kufuatia kupunguzwa kwa misaada kutoka kwa washirika wa kimataifa kama vile Marekani.