1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uchumi

Mkutano wa kilele wa China na Afrika waanza

2 Septemba 2024

China hii leo inawakaribisha viongozi wa mataifa ya Afrika kuzungumzia ushirikiano na mataifa hayo ambayo baadhi yameelemewa na mzigo wa mikopo ya maendeleo na miundombinu, miongoni mwao ikiwa ni Kenya.

Mkutano wa China na Afrika unatarajiwa kuanza Jumanne, Septemba 03, 2024.
Mkutano wa China na Afrika unatarajiwa kuanza Jumanne, Septemba 03, 2024.Picha: Li Tao/Photoshot/picture alliance

China hii leo inawakaribisha viongozi wa mataifa ya Afrika kuzungumzia ushirikiano na mataifa hayo ambayo baadhi yameelemewa na mzigo wa mikopo ya maendeleo na miundombinu, miongoni mwao ikiwa ni Kenya.

Beijing imesema mkutano wa kilele wa China na Afrika ndilo kusanyiko kubwa kabisa la kidiplomasia kuwahi kufanyika tangu janga la UVIKO-19, ambapo idadi kubwa ya viongozi na wawakilishi wanatarajiwa kuhudhuria.

Soma pia: China yazitahadharisha nchi za Magharibi dhidi ya kuitenga kiuchumi

China, taifa la pili kwa uchumi mkubwa ulimwenguni, ni mshirika mkuu wa Afrika katika biashara ambayo ilifikia kiasi cha dola bilioni 167.8 katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, vimesema vyombo vya habari vya China.

Tayari Rais Xi Jinping wa China amekutana na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi na Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, ambao wanatarajiwa kusaini mikataba mbalimbali.

Mkutano huu unafanyika wakati kukiwa na ongezeko la mvutano kati ya China na Marekani juu ya ushawishi na rasilimali za Afrika.