1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele wa EU-China: Nini hasa kilichotokea?

5 Juni 2020

Umoja wa Ulaya na China zimeuharisha mkutano muhimu wa kilele, sababu ikitajwa kuwa ni ugonjwa wa COVID-19. Lakini na maambukizo yamepungua, uchumi unaanzishwa tena kufufuliwa. Je gonjwa hilo ndio sababu ya kweli?

Deutschland China Merkel und Xi PK im Kanzleramt
Picha: Reuters/F. Bensch

Kimsingi mkutano huo ulikuwa na maana kubwa kwa Ujurumani kwa muhtasari ujao wa jiografia ya kisiasa katika nafasi ya urais wa Umoja wa Ulaya. Ni mkutano pekee wa kilele kati ya rais wa China na viongozi wa mataifa 27 ya Umoja wa Ulaya, na ambao mwenyeji wake angekuwa, Kansela Angela Merkel. Mkutano huo wa Septemba ulipangwa kufanyika mjini Leipzig.

Lengo kubwa lilikuwa sio zaidi ya kuufanikisha uhusiano wa Ulaya na China katika mstari nyoofu kwa muongo mpya, kwa kufanyika makubaliano bora, na hasa kwa makampuni ya Ulaya yanayowekeza China na kufanikisha ushirikiano wa karibu zaidi katika makabiliano na ajenda ya mabadiliko ya tabia nchi. Lakini sasa matarajio yamezimwa. Taarifa kutoka kwa msemaji wa wa Merkel inaeleza kwamba pande zote zimekubaliana kwamba " kwa kuzingatia hali jumla ya janga la corona, mkutano hauwezi kufanyika kama ulivyopangwa, lakini pia utapangiwa tarehe nyingine. Hata hivyo hadi sasa hakuna tarehe mpya iliyotajwa.

Kusitishwa kwa mkutano wa kilele kimezusha tafakari nyingi

Mkuu wa ujumbe wa Bunge la Umoja wa Ulaya kwa China Reinhard BütikoferPicha: DW

Hata hivyo tangazo hilo linazusha uvumi mwingi, kwamba kuna mengi zaidi nyuma ya pazia. Pamoja na yote mataifa mengi ya Ulaya yameanza kwa kasi kuondosha masharti ya kukabiliana na virusi vya corona, huku idadi maambukizi na vifo ikipungua. Na kukiwa pia na shinikiza kubwa la ufufuzi wa uchumi. Hata utalii wa kipindi cha kiangazi utawezekana kufanyika katika maeneo mengi ya ulaya. Kwa hivyo katika kipindi cha miezi mitatu, kwa kuandaa mkutano muhimu wa kilele wa namna hiyo kungeweza kufanyika salama kabisa.

Hoja inasalia kwamba Ujerumani ina hofu kuhusu janga la corona, katika kipindi ambacho kumekuwa na mvutano unaotokota katika ya China na Mataifa ya Magharibi. Ni wiki moja tu China iliongeza mbinyo kwa koloni la zamani la Uingereza, Hong Kong, kwa kuridhia sheria mpya ya usalama wa taifa, ambayo inatazamwa kama fursa ya kifo kwa uhuru wa eneo hilo.

Mkuu wa ujumbe wa Bunge la Umoja wa Ulaya kwa China Reinhard Bütikofer, aliambia DW kwamba wanapaswa kuwalinda wanademokorasia wa Hong Kong kwa matakwa yao. Na kuwafikishia mahala panapostahili. Hatua ya China pia imoengeza mgogoro serikali ya taifa hilo na Marekani, na hasa kufuatia kuzuka kwa virusi vya corona. Wataalamu wanasema pande hizo zinaelekea katika Vita Baridi mpya.

Chanzo: DW

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW