Mkutano wa kilele wa G20 kuanza leo mjini New Delhi
9 Septemba 2023Mkutano wa kilele wa kundi la nchi zenye uchumi mkubwa wa viwanda ulimwenguni G20, unaanza hii leo mjini New Delhi. India iliyo mweyeji wa mkutano huo itakuwa na kibarua cha kutafuta mwafaka wa kimataifa licha ya mgawanyiko mkubwa kuhusu vita vya Ukraine.
Kwa kawaida tamko la mwisho na la pamoja ambalo husainiwa na nchi zote washiriki huenda likakosekana kutokana na mitizamo tofauti kuhusu vita hivyo.
Mataifa ya Magharibi, ambayo yameiunga mkono kwa nguvu Ukraine huku yakiiwekea Urusi vikwazo vikali yanaripotiwa kukabiliwa na upinzani wa China na Urusi katika mazungumzo ya G20. Viongozi wa Urusi na China hawahudhurii mkutano wa safari hii na watawakilishwa na mawaziri wa mambo ya kigeni.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi anataka Umoja wa Afrika upewe uanachama wa kudumu ndani ya G20.