Mkutano wa kilele wa mataifa ya BRICS waanza Afrika Kusini
22 Agosti 2023Mataifa wanachama wa BRICS ambayo ni Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini, yanawakilisha robo ya uchumi wa dunia. Nchi kadhaa zimeonesha nia ya kutaka kujiunga na kundi hilo.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amewakaribisha Rais wa China Xi Jinping, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva na baadhi ya viongozi wengine 50. Rais Ramaphosa ameserma Afrika kusini na China zina msimamo mmoja kuhusu swala la kuongeza wanachama wapya.
"Afrika Kusini na China zina maoni sawa kuhusiana na kuongeza wanachama kwenye kundi la BRICS na tunaazimia kufanya majadiliano na viongozi wengine wa BRICS baadaye leo kwenye mkutano wetu."
Mkutano wa kilele wa nchi za BRICS waanza rasmi Johannesburg
Wakati huo huo rais wa Afrika Kusini amesema amejadili juu ya mzozo kati ya Urusi na Ukraine na rais wa China Xi Jinping, katika mazungumzo yao kabla ya mkutano wa BRICS mjini Pretoria.
Kwa upande wake rais wa China Xi Jinping amesema mkutano kati yake na rais wa Afrika Kusini ulikuwa ni wenye tija na kwamba wamebadilishana maoni kuhusu maswala mbalimbali na wamefikia makubaliano muhimu.